MENINAH AMEACHA MAMBO YA WASICHANA

MSANii wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa amejitosa kwenye uigizaji, Meninah amefunguka kuwa anajiona ameshakuwa mwanamke mkubwa hivyo mambo ya wasichana amewaachia wenyewe.

 

Meninah ameliambia Gazeti la ijumaa kuwa kuna kipindi huwa kinafika kwenye maisha kila kitu kinabadilika na mfumo mzima unabadilika na kuwa tofauti na ndivyo alivyo yeye hivi sasa.

 

“Nimekuwa mwanamke kamili hivyo mambo ya wasichana nimeyaweka pembeni, nasimama kama mama ninayejua baya na zuri maana kuna wakati ukifika lazima mtu ungalie lipi la kufanya na lipi la kuweka pembeni,” alisema Meninah.

POSHY AWATAJA WANAOONGOZA KWA CHUKI

MREMBO ambaye alijizolea umaarufu hivi karibuni baada umbo lake kuonekana kuwavutia watu mbalimbali Bongo, Jacqueline obeid ‘Poshy’ amewataja wanawake kama ndiyo watu wanaoongoza kwa chuki na roho mbaya na sio wanaume.

 

Poshy aliiambia Za Motomoto kuwa amegundua kuna wanawake wengi hawapendi kuona wenzao wanaendelea hivyo wataweka kila aina ya chokochoko ili kutibua.

 

“Watu tu wanashindwa kuelewa kuwa huku duniani kila mtu ana bahati yake hivyo ukiona mwenzako anafanikiwa au mwanamke mwenzako anafanya vizuri mshike mkono uzidi kumfanya ainuke ili akuinue na wewe na sio kumponda kila kukicha maana huo unaitwa wivu,” alisema Poshy ambaye tayari amejikwamua kwa kufungua duka lake la kuuza nguo za ndani.

MNYARWANDA WA YANGA ATIMKIA ZAMBIA

KAMA Yanga hawatakaza uzi vizuri basi wapo mbioni kumkosa beki Mnyarwanda, Eric Rutanga ambaye wamekuwa wakimpigia hesabu kwa kiasi kikubwa kutokana na beki huyo kuwa njiani kutua Nkana FC ya Zambia.

 

Rutanga ambaye anacheza nafasi ya beki wa kushoto, ni mmoja wa wachezaji ambao kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera anayetaka asajiliwe na mabosi wa timu hiyo kwa msimu ujao.

 

Rutanga anayeichezea Rayon Sports, anatakiwa na Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu upande wa beki ya kushoto ambapo wapo Gadiel Michael aliyemaliza mkataba na Mwinyi Haji ambaye anaweza kuachwa.

 

Habari za uhakika ambazo Championi Jumatano, limezipata ni kwamba beki huyo anaweza kujiunga na Nkana ya Zambia baada ya kuona dili lake kwenda Yanga likiwa halina uhakika.

 

“Ni kweli kwa sasa Nkana wamekuja kumtaka Rutanga na hali inavyoonekana anaweza kwenda huko kutokana na dili la kwenda Yanga kusitasita.

“Awali walikuwa siriazi na ikaonekana anaenda huko lakini kwa sasa wamepunguza, hivyo beki huyo ameamua kwenda Nkana ambapo wameonyesha nia ya kumtaka,” kilisema chanzo hicho.

 

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela kuhusiana na hilo, alisema: “Tulishamaliza usajili wa kimataifa na ndiyo maana sasa unaona wachezaji tunaosajili ni wa ndani tu. Lakini kama itatokea mwalimu Zahera atasema tumsajili basi tutamsajili kwani hatushindwi kumsajili mchezaji yeyote yule.”

WELLU AFUNGUKA KUZAA WATOTO 4

MSanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo amefunguka kuzaa watoto wanne. akipiga stori na Za Motomoto, Wellu ambaye anadaiwa kuzaa na msanii mwenzake, Steven Mengere ‘Steve nyerere’ amesema kuwa anatarajia kuzaa watoto wanne ingawa hakutaka kumtaja mzazi ambaye atazaa naye.

“Natarajia kuwa na watoto wanne lakini siwezi nikasema hao watoto nitazaa na nani?”Alisema wellu, alipoulizwa kuzaa tena na Steve Nyerere, alibaki akicheka na kukata simu.

MAISHA YA BEN POL KUFURU AINGIA REKODI YA MONDI , KIBA

WAKATI mwingine Mwenyezi Mungu anaweza kukuinua kutoka chini na kukuweka juu! Ndivyo ilivyomtokea staa wa muziki wa R&B Bongo, Benard Michael Paul Mnyang’anga ‘Ben Pol’ ambaye maisha yake kwa sasa ni kufuru kufuatia kumiliki mjengo wa ghorofa.

 

Kwa mujibu wa chanzo, Ben Pol tangu ameanza muziki maisha yake yalikuwa ya kati na kawaida, lakini kwa sasa yamekuwa supa na ni kama ‘amepindua meza’.

 

“Yaani nawaambieni siyo Ben Pol yule aliyekuwa akiishi Kijitonyama, Dar. Maisha yake yalikuwa ya kawaida tu ambayo anaweza kuishi staa wa kawaida anayeanza muziki, lakini kwa sasa hivi jamaa hashikiki kabisa kwani yupo mawinguni. Kwanza leo utamuona amekwea pipa ameenda nchi ile kesho nyingine, kote huko anakula bata,” kilisema chanzo.

MJENGO

Mbali na Ben Pol kuonekana akila bata la hatari hadi kuku wanaona wivu, jamaa anamiliki mjengo wa ghorofa moja ambao upo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar. “Anaishi kwenye mjengo mkubwa wa ghorofa na huo anaumiliki yeye kama Ben Pol.

 

Aliamua kununua kwa sababu ya kurahisisha maisha hata akija na mpenzi wake wa Kenya (Anerlisa Muigai) mara kwa mara ambaye pia ana pesa chafu, basi awe anafikia nyumbani kwake.

 

“Sasa hivi ukifika kwenye mjengo huo utamuona tu Ben Pol anapenda kukaa juu kabisa ambapo kuna uwazi unaweza kumuona mtu yeyote anayepita barabarani,” kilifunguka chanzo hicho.

MAGARI KAMA YOTE

Ukiachilia mbali mjengo huo wa kifahari uliopo ushuani, Ben Pol pia amekuwa akionekana akiwa na magari ya kifahari likiwemo Mercedes Benz ML 350 (M-Class).

 

“Kimjinimjini anatembelea gari aina ya Mercedes Benz ML 350 (M-Class) jeusi hivi, lakini pia wakati mwingine hubadilisha kutokana na eneo analokwenda,” kiliweka nukta chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.

 

BEN POL AFUNGUKA

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Ben Pol anayekimbiza vilivyo na wimbo wake mpya wa Wapo kwenye YouTube alikiri kuishi kwenye mjengo huo na kwamba ni kweli mchumba’ke huyo akiwa Bongo hufikia hapo.

“Ni kweli naishi kwenye mjengo huo wa Mbezi-Beach (Dar) na mchumba wangu akija huwa anafikia hapo,” alisema Ben Pol kwa kifupi.

AINGIA REKODI YA MONDI, KIBA

Kutokana na kumiliki mjengo huo wa kifahari, Ben Pol anaingia katika rekodi ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye anamiliki mjengo Madale, Tegeta jijini Dar na Afrika Kusini huku akiwa amepangisha nyingine sehemu mbalimbali ndani ya Jiji la Dar.

 

Ben Pol pia anaingia kwenye rekodi ya staa mwingine wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ambaye anamiliki mjengo wa kifahari wa ghorofa moja uliopo Tabata jijini Dar.

 

Mbali na Wapo, Ben Pol ambaye ni zao la Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT) ana nyimbo nyingine kali zilizompa umaarufu na shoo za kumwaga ndani na nje ya nchi kama Wakuone, Siyo Mbaya, Nikikupata, Bado Kidogo, Amen, Jikubali, Unanichora, Sophia, Samboira na nyingine kibao.

BLAC CHYNA AICHARUKIA FAMILIA YA ROB KARDASHIAN KISA MTOTO


UGOMVI kati ya mwanamitindo maarufu wa Marekani na ambaye pia ni mwanamuziki, Blac Chyna na Familia ya Kardashian, haujakwisha, hii ni baada ya Blac Chyna kuionya familia hiyo kutotumia jina la mtoto wake Dream katika kipindi chao cha runginga cha Keeping Up With The Kardashians.

 

Chyna alipata mtoto huyo akiwa na mahusiano na Rob Kardashian, lakini baada ya kuachana amekuwa na mgogoro na familia ya Rob kwa madai kijana wao hatoi huduma kwa mtoto huyo.

Hata hivyo Kim, Khloe, Kylie wamekuwa wakimzungumzia mtoto huyo wa kaka yao kwa namna tofauti, lakini Blac Chyna alianza kumuonya Rob kuwa, aiambie familia yake iachane na mpango wa kumzungumzia mtoto wake.

 

Inasemekana kuwa Blac Chyna na yeye anataka kuwa na kipindi chake cha runinga ambacho kitakuwa kinajulikana kwa jina la The Real Blac Chyna, hivyo hayupo tayari kuona mtoto wake akizungumziwa kwenye vipindi vingine.

 

Vipindi vingine vinafanya vizuri kutokana na kutaja majina ya watu, Keeping Up With The Kardashians sitaki kuona wakimzungumzia mwanangu,” alisema Blac Chyna.

ISHU YA FREEMASON… YATIKISA UPYA WASAFI!

KUMEPITA ukimya wa muda mrefu hazijasikika zile habari za msisimko zinazoihusu jamii ya siri duniani inayodaiwa kumuabudu shetani na kuhusishwa na utajiri wa ghafla ambao si wa kawaida ya Freemason hapa nchini, Amani linaibuka nayo.

 

Madai mapya juu ya Freemason inayodaiwa kuhusika na makafara ya damu, yanaigusa familia kubwa ya mastaa wa muziki wa Bongo Fleva chini ya mwavuli wa Wasafi Classic Baby (WCB).

 

Wasafi inajengwa na mastaa wakali walioishika Bongo Fleva wakiongozwa na bosi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’. Wengine ni Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Konde Boy’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ au ‘Chuma’, Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ au ‘Khan’, Abdul Idd ‘Lava Lava’ na first lady wao, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.

WASAFI NA FREEMASON

Madai dhidi ya Lebo ya Wasafi kuhusishwa na Freemason yameibuka upya baada ya jamaa hao kuiteka Bongo kwa shoo kubwa kila kona ya nchi katika Sikukuu ya Idd hivi karibuni. Kufuatia mafanikio hayo, madai ya mtandaoni ni kwamba, jamaa hao wamepata mafanikio ya harakaharaka kwa msaada wa Freemason.

 

Inadaiwa kuwa, mbali na kufunika kwa shoo hizo na kupata utajiri wa ghafla katika siku za hivi karibuni, lakini pia Freemason wanahusika na kung’arisha nyota zao na kuwafanya kukubalika ile mbaya ndani na nje ya Bongo.

 

Katika shoo zao za Idd, Diamond alitikisa Miji ya Kahama na Geita, Harmonize na Queen Darleen wakaujaza Uwanja wa Nangwanda- Sijaona mjini Mtwara na Rayvanny akateka Jiji la Dar katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem. Kwa upande wake Mbosso alifunga mitaa ya jijini Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani huku Lava Lava akifanya kweli mkoani Kigoma kwenye Ufukwe wa Aqua.

TURUDI KWENYE MADAI

Kwa mujibu wa madai ya mitandaoni, wasanii hao wamekuwa wakivaa mavazi, cheni na pete zenye nembo za Freemason kama sehemu ya masharti ya kuwa wanachama wake. “Kinachowaponza ni mavazi yao, cheni na pete zenye nembo za Freemason ambazo huwafanya kung’ara popote wanapokuwa.

 

“Ukiacha mavazi kuna ishara mbalimbali ambazo zinaaminika hutumiwa na Freemason. “Hata salamu zao wanazotumia mara nyingi ni zile zinazotengeneza nembo ya Freemason ya “V” na bikari hasa kwenye kukunja vidole. Hii nayo inawaponza,” kilisema chanzo hicho na kuongeza; “Picha inayotumika kuwahusisha na Freemason ni ile ambayo wanaonekana wote wakiwa kwenye mavazi meusi na pete na cheni zenye alama ya kama msalaba inayoitwa Cross and Crown.

 

“Hii Cross and Crown ni nembo ya Freemason inayomaanisha ushindi dhidi ya kifo. “Kwa kawaida cheni hizo pia huwa na maandishi yanayosomeka ‘In Hoc Signo Vinces’ kwa Kilatini na kwa Kiingereza husomeka ‘By this sign thou shalt conquer’ yakimaanisha kwa alama hiyo watashinda,” kilisema chanzo cha karibu cha mastaa hao wa Wasafi.

MENEJA AFUNGUKA

Mmoja wa mameneja wa Wasafi aliyezungumza na Gazeti la Amani juu ya ishu hiyo, Said Fela alianika ukweli wa anachokijua juu ya jambo hilo.

 

“Kwenye mafanikio ya wasanii wetu yanasemwa mengi, wengine wanasema tunaloga na wengine hayo mambo ya Freemason, lakini ukweli hakuna kitu kama hicho. “Siri ya mafanikio ya Wasafi ni kujituma kwa wasanii na uongozi makini hayo mengine hayana ukweli wowote,” alisema Fela.

 

DIAMOND NA FREEMASON

Ukiwaacha memba wengine wa Wasafi, lakini miaka kadhaa Diamond alihusishwa na Freemason ambapo aliwahi kufafanua suala hilo kupitia magazeti pendwa yanayoongoza kusomwa na wengi nchini Tanzania ya Global Publishers ambapo alisema; “Ni stori tu ambazo hata mimi nazisikia kama wewe (mwandishi), lakini sifahamu chochote juu ya mambo ya Freemason.”

 

FREEMASONI NI NINI?

Freemason ni jamii ya siri inayohusishwa na dini ya kishetani na watu wengi maarufu wanatajwa kuwa humo wakiwemo viongozi wa nchi mbalimbali na mastaa wengine kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye West na Celine Dion.

KITALE NOMA! AWAJIBU JOTI, MASANJA KWA MJENGO WA MAANA

BAADA ya maneno mengi kuwa tasnia ya filamu Bongo hailipi, staa wa vichekesho, Yusuph Mussa Kitale ‘Mkude Simba’ au Rais wa Mateja’ ameangusha mjengo wa maana na kuondoa kabisa mawazo kwamba tasnia hiyo hailipi. 

Hadi hapo ulipofikia kabla ya finishing (kumalizika kabisa), mjengo huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 78.

 

Kitale anayerusha vichekesho vyake kupitia Radio EFM amewajibu mastaa wa vichekesho wanaotamba kwa mijengo mikali Bongo kama Lucas Mhuvile ‘Joti’ na Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’. Kama ilivyo kwa Joti na Masanja, mjengo wa Kitale nao upo Kigamboni, eneo la Kibada jijini Dar.

 

Joti na Masanja wanamiliki mijengo ya kifahari ya ghorofa mojamoja maeneo ya Kigamboni jijini Dar. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda juu ya mjengo huo, Kitale alisema anatarajia kuhamia kwenye mjengo huo mara tu utakapomalizika kwa kuwa upo katika hatua za mwisho.

“Nitahamia mara tu nitakapomaliza kuujenga maana upo katika hatua za mwisho na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 78 za Kitanzania.

 

“Sanaa ambayo ninafanya (uigizaji wa vichekesho) ndiyo imeniwezesha kujenga kwani sina kipato kingine zaidi ya sanaa ila kikubwa ni kuweka malengo na ukiweka malengo ya kufanya kitu na ukaweka nia pia utafanikiwa

“Ninachojua mimi hakuna pesa ndogo kama utaifanyia kile ambacho umekusudia.

“Kwa hiyo mimi kwa upande wangu sanaa inalipa na ndiyo maana nimefanya hivi na natarajia kufanya vitu vikubwa zaidi. Kipaji changu ni sanaa, ninafanya kwa kadiri ambavyo itaniletea manufaa,” alisema Kitale ambaye pia amefanya filamu nyingi za vichekesho kama Chizi Kalogwa Tena, Simu ya Kichina, Bwege Mtozeni nk.

WATUMISHI WAWILI TARURA WAFARIKI AJALINI SONGWE

WATUMISHI wawili wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Road Agency – TARURA) wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea Izazi katika Barabara Kuu ya Iringa-Dodoma baada ya gari lao kugongana na lori lililohama upande baada ya kumshinda dereva wake.

 

TAARIFA YA POLISI

Mnamo tarehe 25.06.2019 majira ya 05:45 hrs maeneo ya Izazi kata ya Izazi tarafa ya Ismani wilaya ya Iringa na mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Iringa-Dodoma.

 

Gari lenye namba za usajili STL 3807 aina ya Toyota Hilux, mali ya TARURA,  likiendeshwa na Lodrick s/o Richard@Ulio, miaka 35, kabila Mchaga na mkazi wa DSM likitokea Iringa kuelekea Dodoma liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T 146 BAZ aina ya Mitsubish Fuso mali ya Wilson S/o Msenga wa Iringa likiendeshwa na Amos s/o ??? wa Iringa likitokea Dodoma kuelekea Iringa.

 

Madhara

VIFO

1. Lodrick s/o Richard@Ulio-dereva wa TARURA

2. Joyce d/o Enezar@Mlay, miaka 45, kabila Mchagga mkazi wa Moshi.

MAJERUHI

1. Ernest s/o Mgeni, miaka 49, kabila mkinga na mkazi Mbozi

2. Gervas s/o Myovela, miaka 44, kabila mhehe mkazi wa Mbozi

3. Jamadin s/ Mikata, miaka 32, kabila mngoni na mkazi wa Mbozi

Wote walikuwa kwenye gari la TARURA na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Iringa kwa matibabu.

Aidha, miili ya marehemu imekabidhiwa kwa meneja wa TARURA manispaa Iringa na kupekekwa Dodoma tayari kwa utaratibu wa mazishi.

 

Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Fuso kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhama upande mmoja na kugongana uso kwa uso ambaye amekimbia mara baada ya ajali hiyo na anatafutwa.

 

WITO

Madereva wawe makini wanapotumia barabara wasijione wako peke yao bali waheshimu sheria na watumiaji wengine wa barabara.

ROSTAM AFUNGUKA KILICHOMRUDISHA NCHINI, AMTAJA MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz alipowasili kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Ltd. mfanyabiashara Rostam Aziz, amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuweka usawa wa kibiashara katika miaka minne ya uongozi wake.
Aidha, mfanyabiashara huo ameahidi kuwekeza katika miradi mingine zaidi nchini itakayogharimu zaidi ya Sh bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz kuangalia Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo kabla ya kuvizindua huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

Rostam amesema hayo leo Jumanne Juni 25, Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ghala na mitambo ya gesi ya taifa (Taifa Gas) ambayo ni gesi ya majumbani iliyozinduliwa rasmi na Magufuli.
Amesema mafanikio ambayo wao kama Taifa Gas na makampuni mengine kutoka nje wanayaona yanatokana na kazi kubwa aliyoifanya Magufuli tangu aingie madarakani mwaka 2015.

Rais Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

JPM, ROSTAM AZIZ KATIKA UZINDUZI WA GHALA KIGAMBONI

“Uimarishwaji wa sekta binafsi utatekelezwa kwa uwanja ulio sawa kama kujenga miundombinu itakayowasaida Watanzania kujikwamua kutoka katika umaskini wa kihistoria na mheshimiwa Rais historia itakukumbuka katika hili,” amesema Rostam.

Rais Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

“Kuna watu walisema kuwa wewe si rafiki wa sekta binafsi,  nataka niwaambie kuwa uongozi wako ndiyo umefanya nianze kurudisha mitaji ya uwekezaji ambayo niliwekeza nje, na Taifa Gas ni mwanzo tu ila kuna miradi mingine itakayogharimu Sh. bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo,” amesema.

Rais Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG.