MREMBO Tessy Abdul ‘Tessy Chocolate’ ametoa kauli tata inayotafsiri kwamba anamzungumzia mzazi mwenziye, Aslay Isihaka japokuwa hakutaka kumtaja moja kwa moja. Akizungumza mawili-matatu kuhusu maisha yake kwa jumla mbele ya kinasa sauti cha Amani, Tessy alichomekea kuwa, watu wasiwe na wasiwasi pindi inapotokea wamepoteza kitu maishani kwani yeye amejifunza kama Mungu akipanga utakuwa na kitu hata kama kikipotea ipo siku kitarudi tu.

“Watu wengi utakuta wakilaumu vitu mbalimbali kwenye maisha yao vikiondoka, lakini wanasahau kuwa kitu kama kikiondoka kwenye maisha yako na hakikurudi tena, basi Mungu amepanga, lakini kama alisema ni chako, kitarudi tu bila tatizo lolote,” alisema Tessy huku akiachia tabasamu na alipoulizwa kama kauli hiyo inamaanisha anaweza kurudiana na Aslay hakutaka kuweka wazi.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *