Kuna wale vijana magraduate ambao hawapendi kuishi huku kwetu Uswahilini. Wewe umeanza kazi mshahara unapata 1.2 m baada ya makato, una somesha wadogo zako wawili na wazazi wanakutegemea wewe kule Kibondo bado unaleta jeuri mjini.

Loading…

Sikuhizi vyumba vinapangishwa kwenye family house Mbezi Beach hata Mikocheni. Unamkuta aunty ana watoto wanne wawili wakubwa wako Marekani na hawa wadogo wako boarding English Medium. Aunty anapangisha kwa sababu za ki usalama hasa akiwa safarini.

Unaambiwa chumba 50,000 kwa mwezi pamoja na umeme na gesi humo humo. Ma aunty huwa hawapendi wapangaji wa kike hasa yule anaelijua jiko mpigane vikumbo bure jikoni. Wanapenda young men huwa hawana time sana na jiko.

Umehamia Mikocheni na washkaji hawakumalizi maana pamoja na vyuma kukaza kodi ya kupanga nyumba nzima Mikocheni si utani

Mara umetoka kazini unakuta pilau na soda ya baridi. Kesho unakuta chapati, mchuzi wa kuku na mchicha. Mtondo ndizi nyama. Unajifikiria jinsi ya kurudisha wema huu. Unaamua kumnnunulia aunty wine. Unamkuta sitting room akiwa na khanga moja….Nadhani mpaka hapo stori hii unaweza imalizia Mwenyewe…..

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *