PAMOJA na kwamba aliposepa Bongo na kutimkia mamtoni (Marekani), staa wa Bongo Muvi; Diana Kimari, alisema hawezi kurejea, lakini ukweli ni kwamba nyumbani ni nyumbani kwani sasa amepakumbuka mno na anatamani kurejea.

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu akiwa Marekani, Diana anasema amemkumbuka mno mama’ke na baadhi ya rafiki zake ambapo huko hawapo, hivyo hapawezi na anatamani mno kurejea Bongo. “Kiukweli nimemisi sana nyumbani na natamani kurudi,” alisema Diana.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *