SEXY lady kunako Bongo Flevani, Faustina Charles ‘Nandy’, anaendelea kulamba madili ya mamilioni kama yote. Wiki iliyopita alisaini mkataba wa dili lingine na Kampuni ya Azania Group kuwa balozi wa sabuni yake mpya iitwayo King Limau na King Marhaba.

Kampuni hiyo ambayo awali ilikuwa ikijihusisha na bidhaa za chakula, imetoa sabuni hiyo ya unga iliyoelezwa kuwa na ubora wa kimataifa. Baada ya kutiliana saini za mkataba wa kuitangaza bidhaa hiyo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hytt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar, Nandy aliliambia Ijumaa Wikienda;

“Nilianza kutumia sabuni hizi wiki tatu zilizopita na kujidhihirishia ubora wake, ndiyo maana nimekubali kuwa balozi wake.” Mbali na dili hilo, Ijumaa Wikienda linafahamu kuwa Nandy pia ana madili mengine makubwa likiwa la kampuni kubwa ya vinywaji, kampuni ya simu na bidhaa zenye jina lake

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *