DUNIA ina mambo! Baada ya picha akiwa amembeba mgongoni mumewe Said Mtopali kuzagaa mitandaoni na kuzua gumzo, msanii wa Bongo Fleva, Mascat Aboubakar ‘Amber Rutty’ ameeleza kuwa anatamani kumbeba mwandani wake huyo kichwani.

 

Akistorisha na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Amber Rutty alisema anashangaa watu kupigwa butwaa yeye kumbeba mumewe mgongoni wakati kwake ni jambo la kawaida kwani kutokana na jinsi wanavyopendana anatamani kumbeba kichwani.

 

“Kwa jinsi ninavyompenda mume wangu na tunavyopendana natamani kumbeba kichwani, sema tu kichwa kitaniuma lakini isingekuwa hivyo ningembeba ili kuonesha thamani ya upendo wangu kwake,” alisema Amber Rutty.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *