DKT. Donna Francis amekiri mashtaka ya mauaji yaliyotokana na uzembe baada ya kumfanyia upasuaji mwanamke (34) ambaye alienda kwake kwa ajili ya kuongeza makalio nchini Marekani.

Donna ambaye hana leseni ya kufanya shughuli za kitabibu alikuwa akifanya upasuaji wa kuongeza maumbile kwa mwanamke huyo mnamo Mei 2015, ambapo wakati wa upasuaji mgonjwa alipatwa na mshtuko wa moyo uliopelekea kupoteza uhai wake.


Inaelezwa kuwa kifo cha mwanamke huyo kilisababishwa na dawa ya kuongeza maumbile ambayo alichomwa na daktari wakati wa upasuaji. Hukumu yake itatolewa Novemba 14, mwaka huu.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *