WAKATI stori zikien­delea kusambaa mitandaoni ame­chukuliwa mumewe na mwigizaji Eliza­beth Michael ‘Lulu’, mke wa msanii wa Bongo Fleva, Ray­mond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ‘Fayvan­ny’ ameanika kinachoende­lea.

 

Tetesi za bifu la Lulu na Fayvanny ziliaza kusambaa wiki kadhaa zilizopita ikidaiwa kwamba eti walikutana saluni na kutaka kuzichapa kavukavu.

Kufuatia ishu hiyo, Shusha Pumzi ilizungumza na Fayvanny ambaye anasema kwa kifupi kuwa hahitaji kulipa jambo hilo kiki isiyokuwa ya lazima.

“Iwe ni kweli tulitaka kupigana au la, sipo tayari kuliongelea jambo hili kwa sasa kwa sababu limeshapita, nikianza kuliongelea, nitakuwa kama nazidi kulipa nafasi ya watu kuliongelea. Pia sihitaji kumuongelea sana huyo Lulu kwa kuwa hayo mambo yalishapita na sasa hivi naishi vizuri tu na mume wangu,” alisema Fayvanny.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *