MWANAMITINDO maarufu Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ ametaja sababu za kufanya bethidei yake kimya kuwa hakutaka makuu badala yake alipeleka misaada mbalimbali kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Akipiga stori na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Poshy ambaye kwa sasa ni mjasiriamali wa nguo za ndani alisema aliona akisherehekea kwa kula na kunywa vizuri na rafiki zake hakuna faida yoyote, badala yake aliona apeleke misaada mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji hospitalini hapo.

 

“Kama kufanya sherehe nyingi siku yangu ya kuzaliwa nimeshafanya sana au kutoka na marafiki nimetoka sana, sasa nimeona bora tu nirudishe wema alionitendea Mungu kwa kuwasaidia wenye mahitaji,” alisema Poshy.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *