THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)

ILIPOISHIA: “Kumbe wakati napanda kwenye ule mti, mmoja kati ya walinzi wa eneo hilo, alikuwa ameshaniona na akawa anasubiri aone mwisho wangu. Nikiwa pale chini, nilishtukia bomba la baridi likinigusa shingoni, likifuatiwa na sauti ya ‘tulia hivyohivyo kwa usalama wako)’, nikajua nimepatikana. SASA ENDELEA… Miongoni mwa vitu ambavyo Mungu amenijaalia, ni kutokuwa na hofu au […]

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 3

ILIPOISHIA: “Inuka na ufanye ninachokueleza, ukizingua unajua nini kitatokea,” nilisema kwa sauti ya chini lakini yenye mamlaka, yule mwanamke akakurupuka akiwa ni kama haamini kilichotokea, Suma naye akawa anatetemeka akiwa haelewi nimeingiaje pale. SASA ENDELEA… “Snox! Nakuomba mdogo wangu, please show me some mercy!” (Nionee huruma tafadhali) alisema Suma huku akiwa anatetemeka kuliko kawaida lakini […]

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 2

ILIPOISHIA: Bado nilikuwa nazikumbuka namba za siri nilizotumia kukifunga, macho yangu yakatua juu ya kitu kilichosababisha nitabasamu! Siyo tabasamu la furaha, la hasha! Tabasamu la kifo, tabasamu ambalo huwa linaonekana usiku wa giza totoro pekee. SASA ENDELEA… Unaweza kujiuliza nilikuwa nimeona nini kilichosababisha nitoe tabasamu la aina hiyo? Kihulka mimi ni mpole sana na pengine […]

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

“Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimesema fungua! Fungua kwa hiyari yako!” “Huyo ni nani?” “Shiii! Rudi ndani kalale!” “What is going on? Please let me know!” (Nini kinaendelea? Tafadhali naomba nieleweshe). “Ngo! Ngo! Ngo!” Kufumba na kufumbua, kishindo kikubwa kilisikika, mlango ukaja kunibamiza kwa nguvu na kunirusha mpaka ukutani, nikajibamiza […]

THE DARKENED SOUL (NAFSI ILIYOPATWA NA GIZA) – 01

Posta, Dar es Salaam. Kishindo kikubwa na kizito kilisikika eneo lote na kusababisha mpaka majengo yatingishike utafikiri kumetokea tetemeko la ardhi, watu waliokuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida, waliacha kila kitu na kuanza kukimbilia mahali kishindo hicho kilikotokea, kila mtu akiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ni nini hasa kimetokea. “Ameua! Ameua!” “Kwani […]

INSANE (MWENDAWAZIMU)-12

ILIPOISHIA Ukawa mwanzo, wakaanza hivyo. Theo hakutaka kuacha, alichoamua kilikuwa ni kumpoteza kabisa Fabian moyoni mwa msichana huyo. Hiyo, haikuwa kazi nyepesi kwani wakati mwingine alimfurahisha Esther lakini alipopita Fabian, msichana huyo alinyamaza na kumwangalia mwanaume huyo, alitamani kumuongelesha lakini aliamua kunyamaza tu. “Kuna nini?” aliuliza Theo huku akijua kabisa kilichokuwa kikiendelea. “Naomba tuondoke hapa!” […]

INSANE (MWENDAWAZIMU)-11

ILIPOISHIA “Ni nani anamfanya huyu msichana kunichunia hata nikimsalimi? Au hajui kama mimi ni mtoto wa bilionea? Subiri! Nitamfuata tu na si kuishia kumsalimia,” alijisemea, wakati akizungumza hayo, miguu aliweka juu ya meza ambapo hapo kulikuwa na mabunda ya hela aliyokuwa ameyapanga. Kwa hesabu za harakaharaka zilikuwa kama milioni kumi na tano. Wanafunzi wote wakawa […]

INSANE (MWENDAWAZIMU)-09

ILIPOISHIA Boniface akashtuka, hakutaka kubaki ndani ya ofisi yake, akateremka kwenye ngazi harakaharaka, alipofika chini, akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa mahali hapo. Aliwaona watu hao kwa mbali lakini hakuweza kuwapata kwani kulikuwa na foleni kubwa ya magari, akajikuta akikwamishwa na magari hayo. Pikipiki hiyo ilipofika maeneo ya Stesheni, ikakata kulia na kutokomea huko […]