Hajui Kama Nimeoa, Penzi Limenoga Nataka Kusema Ukweli Lakini Sujui Nianzie Wapi

Sijawahi kuwa mzinzi tangu nimeoa miaka 5 iliyopita. Hadi hivi karibuni nilipoanzisha uhusiano na binti mmoja..

Tulifahamiana kikazi, yeye yupo idara ya uhasibu. Huja kazini kwangu kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya transaction mbalimbali.

Tukazoeana na kuwa wapenzi. Kiukweli mambo yalienda haraka haraka sana na aliingia mazima mazima kiasi kwamba hata kila nilipotaka kumwambia ukweli najikuta nashindwa maana alikua resi ile mbaya.

Ikawa ni mahaba niue, kila tukitoka kazini tupo wote sehemu, weekend tutaenda cinema, beach etc. Yaani ghafla bin vuu anaongelea ndoa. Kila siku ya Mungu lazima agusie ndoa itakua vipi.

Wakati mwingine anaingia Google kusearch magauni ya harusi na viatu na maids wake watavaa nini siku hiyo. yaani nabaki mdomo wazi maana moyoni najua nimeshaoa siku nyingi.

Kila akianzisha hizo story za magauni najitutumua sasa nianze kumwelewesha kwamba nimeoa basi hunikata kauli haraka na kuendelea kusema mambo ya ndoa yetu kwamba napendelea ukumbi gani ndo mzuri.

Sasa tuna miezi miwili ameanza kuongelea suala la kupata mtoto ananiuliza kuwa naonaje akibeba mimba kabisa tufunge ndoa wakati ana mimba. Basi humjibu kuwa tusubiri kwanza asibebe kabisa mimba, nikijibu hivyo anakua mkali anauliza “hiyo mimba unaibeba wewe au mimi?” Mimi nabaki kimya.

Kwa kweli namuonea huruma kwa mawazo aliyonayo, mimi niliingia kwenye huu uhusiano kubadilisha mboga tu and I thought it would be a temporary thing. Kiuchumi yupo vizuri balaa simpati hata kwa dawa.
Ukifika alipopanga thamani za vitu alizonazo ndani ni za gharama sana, na nyumba ni ya kisasa, ana miradi mingi mbali na kazi na alinipeleka anapojenga nyuma ni kama imeisha bado ukuta tu wa nje.

Tatizo pekee ninaloliona ni kuwa huyu binti time is ticking very fast against her age, yupo kwenye mid 30s; somewhere between 30-36 years. Hivyo anadhani amechelewa.

Anasema amepoteza muda mwingi kwenye relationship iliyopita iliyochukua 7 years na jamaa akaoa mtu mwingine na kumuacha yeye, hivyo anasema hataki tena long relationship. Ameshaniunganisha na ndugu kibao. Kila wiki natambulishwa kwa ndugu mpya.

Wakuu, naona huruma Kubreak hii news kuwa nilishaoa. Ingawa nampenda moyoni lakini pia nimechoka maisha ya digi digi ninayoishi maana nikiwa home kwangu usiku lazima anipigie simu na anaongea zaidi ya nusu saa na hapo tumetoka kuonana jioni. Basi najifanya naenda dukani kwa mangi kununua kitu na kupiga stori ili wife asishtuke kuwa naenda kuongea na simu.

I think wengi mnajua maisha ya Ku,cheat yalivyo magumu ni utumwa, ni jela ya nje.

Wakuu nianzeje kumwambia ukweli anielewe? Au nitume mtu mwingine ndo amwambie kama anampa umbea vile?

Wanaume Waongeza Safari Kukwepa Michepuko

UDANGANYIFU kwa ‘michepuko’ miongoni mwa wanaume wengi siku hizi ni mwingi kama ambavyo tumekuwa tukiangazia kwa wiki tatu mfululizo.

“Simu yangu imejiblock siwezi kutuma hela kwa sababu ziko kwenye simu.”

“Nimetoka kumuuguza mama yangu, nimerudi siko vizuri kifedha.”

 

“Ntakutumia hiyo hela kesho,” lakini hatumi kama alivyoahidi.

Ni miongoni mwa sababu ambazo zimewafanya wanawake wengi ambao walikuwa wakiendesha maisha yao kwa kutegemea kuhongwa kuachana na mategemeo hayo.

 

Wanaume waliokuwa wakionekana kuwa ni ‘Ma-Kassim’ wakiingia mbaa wanaagiza ‘lete kama tulivyo’ wamepungua, wengi wao jeuri ya fedha imekwisha; wamekuwa watiifu kwenye ndoa zao.

Jambo hili kama tulivyoangalia wiki liyopita ndilo lililowasukuma wanawake wengi siku hizi kuamua kujitafutia maisha ili kulinda heshima zao.

 

Kama alivyosema Andrew wiki iliyopita kuwa: “Haya ni mapinduzi makubwa kwa wake zetu, walikuwa wamembweteka, hawataki kufanya kazi kwa sababu walikuwa wanaletewa kila kitu, leo hii hali si shwari; nao wamelazimika kuingia mitaani kufanya biashara.”

 

Hata hivyo hakuna mageuzi ya kiuchumi yasiyokuwa na mtikisiko, wakati wasichana waliokuwa wakichukuliwa kama nyumba ndogo za baadhi ya ‘wapiga madili’ siku za nyuma kuathirika kwa kukosa udambwidambwi wa kuhongwa, familia za akina ‘Kassim’ waliofilisika nazo haziko salama.

 

Uchunguzi wa OFM unaonesha kuwa, kushuka kwa pato katika familia zilizokuwa zikiishi ‘kifalme kwa kula wanachotaka na siyo kula wanachopata nazo zimetikisika.

 

Migogoro mingi imeibuka kwenye ndoa; sababu kubwa ni kushuka kwa pato la familia, wanaume wengi wameanza kulia kusalitiwa na kudharauliwa na wake zao.

“Mke wangu amebadilika kabisa kitabia, tofauti na zamani, jeuri imekuwa kubwa mno kiasi kwamba nahisi amepata mwanaume nje ya ndoa.”

 

James (jina la utambulisho tu) mkazi wa Kimara Baruti jijini Dar es Salaam, alimwambia mmoja wa wachunguzi wetu jinsi ambavyo anahisi mke wake amebadilika kitabia.

 

Alipouzwa kwa nini mke kabadilika kitabia alisema: “Unajua wake zetu kipato kikishuka na mapenzi yanashuka,” alisema James akimtaja mkewe kama mwakilishi wa wanawake wote jambo ambalo si sahihi kusema “WAKE ZETU,” ni bora angesema mke wake!

 

Hata hivyo, uchunguzi uliowahi kufanywa awali na timu yetu ya OFM kuhusiana na SABABU ZA WANAUME KUUA WAKE ZAO KWA WIVU WA KIMAPENZI ulibaini kuwa wanaume wengi wamepoteza hadhi zao hasa baada ya wanawake kuamka kimaisha.

 

Hali ya wanawake wengi siku hizi kuacha tabia za kutegemea kuletewa na wanaume zimewafanya wawe majasiri jambo ambalo linachukuliwa na baadhi ya wanaume kuwa ni dharau kwao kama ambavyo James alivyojaribu kulinganisha kushuka kwake kimapato na kudharauliwa na mkewe.

 

Kama ambavyo tumesema mageuzi yaliyofanyika kichumi miongoni mwa wanawake na wasichana wengi kuanza harakati za kujitafutia maisha kumezua mtikisiko mkubwa kwenye familia.

 

“Yaani mume wangu siku hizi wivu umepita kiasi kila nikichelewa kurudi ugomvi hauishi, hata nikimwabia kuwa biashara ndiyo imenichelewesha haniamini anasema nilikuwa kwa wanaume zangu,” alisema Khadija mkazi wa Keko, Dar alipozungumza na OFM walipokuwa katika uchunguzi.

 

Hali halisi iliyoonekana baada ya kuchunguza kwa makini ni kuwa, wanaume wengi ambao wanawake zao wameamua kuanza kufanya biashara wamekuwa wakiteswa na mambo kadhaa muhimu.

MOJA ni ile hali ya wanawake kuacha utegemezi jambo ambalo linawafanya wanaume kujiaminisha kwamba huwenda wake zao wamepata wanaume wengine wanaowategemea tofauti na wao.

 

PILI; ni muda wa wanawake kuwepo nyumbani. Wengi kati ya wanawake wanaofanya biashara wamekuwa wakitoka nyumbani mapema na kurudi jioni au usiku.

Kutokuwepo nyumbani kwa saa nyingi kumewafanya baadhi ya wanaume kuwa na mawazo potofu kuwa huwenda wake zao wanatumia kisingizio cha ‘kufanya biashara’ kujihusisha na usaliti katika ndoa.

 

TATU; wanawake kuwa na kipato wakati mwingine kikubwa kuliko wanaume kunasababisha kuwepo kwa mashaka ya uhalali wa upatikanaji wake na wakati mwingine kuonekana kama ni ‘jeuri’ kwa wanawake.

“Nafanya biashara zangu najipatia fedha kidogo namsaidia mume wangu kuendesha maisha ya familia, lakini hatosheki, yaani kitu kidogo tu anakimbilia kusema pesa zinanipa kiburi.

 

“Sasa zinanipa kiburi kwani nazitumia peke yangu? Kila nikipata nahudumia familia na wakati mwingine hata yeye namnunulia nguo na mahitaji mengine,” alisema Mwanahawa mkazi wa Mbagala Rangi Tatu jijini Dar.

NNE; wanawake kutumia muda mwingi kwenye kazi na kurudi nyumbani wakiwa wamechoka na hivyo kushindwa kuwajibika ipasavyo kwenye masuala ya ndoa.

 

“Huyu mwanamke kuna mtu anamshika masikio, haiwezekani; mimi ananichukulia kama mtu wa ziada kwake, hata tendo la ndoa ananipa siku akijisikia, muda mwingi yeye kachoka,” Frank wa Kigamboni alilalamika.

Wapenzi waliogombana, tiba ni hii hapa

 KUGOMBANA ni jambo ambalo halikwepeki katika uhusiano wa kimapenzi. Upo ugomvi ambao ni wa kawaida na huisha kirahisi lakini upo ugomvi ambao huwa mkubwa na kama ukitokea na ukashindwa kujua nini cha kufanya ili kuweka mambo sawa, husababisha ufa kwenye penzi lenu.

Leo nitazungumzia mambo muhimu ya kufanya inapotokea wewe na mpenzi wako mmeingia katika ugomvi, mmetoleana maneno machafu au hata kupigana. Kwanza, tafakari chanzo cha tatizo. Kuna usemi kwamba ukitaka kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza ujue chanzo cha tatizo lenyewe. Ukishindwa kugundua chanzo cha tatizo, basi na wewe unakuwa sehemu ya tatizo.

Utashangaa kwamba wapenzi wengi hugombana na mambo kuwa makubwa kabisa kwa sababu ya vyanzo vidogo ambavyo walishindwa kuvigundua mapema na matokeo yake vikazaa matatizo mengine. Mfano rahisi, chanzo kinaweza kuwa mpenzi wako amekupigia simu lakini ukashindwa kuipokea kwa muda muafaka. Atakapopiga kwa mara nyingine au mkikutana, usitegemee atakufurahia kwa sababu atahisi umemdharau kwa kutopokea simu yake.

Endapo utafanya makosa ya kushindwa kuliona kosa lako mapema na kushindwa kuomba radhi au kutoa maelezo yanayoeleweka kwa nini hukupokea simu, matokeo yake utamjibu vibaya, naye atakujibu vibaya na mwisho mtaishia kupigana au kuachana kabisa mkiwa mmeshatoka kabisa kwenye kosa la msingi. Bila shaka msomaji wangu umeona jinsi chanzo kidogo kinavyoweza kusababisha tatizo kuwa kubwa. Ndoa nyingi au uhusiano unaofika mwisho huwa umesababishwa na mambo madogo ambayo yalishindwa kutafutiwa suluhu mapema.

Katika kila ugomvi unaotokea, jambo la kwanza jipe muda wa kutafakari chanzo kilichosababisha mkagombana. Wakati mwingine wewe ndiye unaweza kuwa chanzo cha tatizo lakini kama ukiyajua makosa yako mapema na kukiri kisha kuomba radhi kwa mwenzio, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kurudisha mapenzi kwa haraka.

Pili, mpe muda ili hasira zake ziishe. Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni wachache wanaoweza kuzidhibiti hasira zao. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga au kuharibu vitu akiwa na hasira.

Baada ya kugombana, kila mmoja lazima atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi, ni kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira zipungue. Tatu, mpe nafasi ya kutoa lililo moyoni mwake. Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na kumaliza kile alichokusudia kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua za kusaka suluhu, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku lililopo ndani ya moyo wake.

Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi mpaka dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa upole na sauti tulivu. Nne, ni busara zaidi kuomba msamaha. Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote na kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha. Neno ‘samahani’ ni dogo lakini lina maana kubwa kwa yule mtu anayelitoa na anayelipokea.

Hata kama unaona dhahiri kwamba kosa siyo lako, omba msamaha kwanza kisha baada ya hapo anza kumuelewesha mpenzi wako kwa upole. Lazima mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza kuepuka kuukuza ugomvi huo na kurudisha hisia za mapenzi.

Je, Ntakuwa Nimemuharibu Mtoto? Nimefanya Mapenzi na Mwanaume Ambaye si Baba wa Mtoto…

Mimi nina mtoto wa miezi 10 sasa, niliachana na aliyenipa ujauzito nikiwa na mimba ya miezi 2 mwaka jana mwezi wa 2, na tangu mwaka jana nilikua sijakutana kimwili na mwanaume yoyote yaani nimekaa mwaka 1 na miez 5.

Miezi mitatu iliyopita nilikutana na kaka mmoja akawa anataka kunioa, but juzi nikashiriki nae tendo kibinadamu, na mimi na hisia kweli.Nilisex nae mara 1 tu na nilienda kuoga kabla sijamnyonyesha mtoto.

Naomba kuuliza inaweza kumdhuru mtoto?

Je, nifanyeje?

Msinielewe vibaya ndugu yangu baba mtoto yuko mbali na ana mwanamke mwingine .

Hana muda na mimi kabisa, mimi ni binadamu hisia zilinizidi tu nikawa nimefanya hivyo.

Amber Lulu Aanika Alivyoshea Bwana na Gigy!

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amefunguka suala la kushea bwana na msanii mwenzake, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

Amber Lulu amesema kuwa, ni kweli aliwahi kushea mwanaume mmoja na Gigy Money siku za nyuma.

 

“Kutokana na lifestyle yangu ya sasa hivi, watu hawamjui bwana’ngu kwa hiyo wanajitahidi kumtafuta na kuotea kama natoka na nani.

“Mimi sijawahi kugombana na mtu, hizo stori za kugombea mwanaume ni zamani sana, kama miaka mitatu au miwili huko nyuma.

 

“Nakumbuka mwanaume ambaye mimi nilipita naye na yeye (Gigy) akapita naye ni Casto Dickson,” alisema Amber Lulu.

 

Msanii huyo amezungumzia suala la wanawake kudanga ili wapate pesa ambapo amesema kuwa.

“Inatokeaga mara nyingi sana, Bongo hakuna mwanamke awe na mtu halafu akatae pesa, kila mtu anategemea mwanaume mwenye pesa, halafu sisi wanawake tunapenda kupewa ila inategemea unadanga kiasi gani,” alisema Amber Lulu.

Mke wa Rayvanny Abanwa Kumkuwadia Mondi

UKISIKIA mambo ni moto ndiyo haya sasa! Wakati mwandani wa mwanamuziki wa kimataifa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna akiwa leba akijifungua hivi karibuni, uliibuka ubuyu matata kuwa jamaa huyo anachepuka.

FAHYMA MFANIKISHAJI

Huku na huku ikaelezwa kwamba facilitator (mfanikishaji) wa ishu hiyo ni mke wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambaye Diamond ni bosi wake pale Wasafi, Fahyma ‘Fayvanny’ ambaye alikuwa akimkuwadia mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa Diamond au Mondi. Mambo yakawa ni mengi na mji ukawa mzito kuwa, Fahyma ni rafiki mkubwa wa Hamisa hivyo alitaka kumrejesha kwa Mondi ambaye alishakuwa naye zamani na wakafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Dyllan.

TANASHA  ALIPONYAKA ISHU

Kwa upande wake, Tanasha wakati akifurahia kupata mtoto wa kiume na Mondi huku akisota leba pale Hospitali ya Aga Khan jijini Dar kwa saa takriban 17, alipotoka hospitalini akafikishiwa ishu na kumsababisha kucharuka kinoma. Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti hili, zilipita siku kadhaa, Tanasha na Mondi wakawa hawaelewani kama mwanzo kwa sababu ya meseji za kimapenzi zilizodaiwa kunaswa.

Ilidaiwa meseji alizonasa Tanasha kwenye simu ya Mondi zilikuwa zinatoka kwa Hamisa. “Kiukweli mapenzi ya Mondi yaliyumba mno kiasi cha kupumulia mashine. “Watu walikuwa wanamuonea huruma yule binti wa watu kutokana na mambo yaliyokuwa yanamtokea huku akiwa ndiyo kwanza ametoka kujifungua.

MONDI NA HAMISA TENA?

“Ishu kubwa ilikuwa inasemekana eti jamaa (Mondi) alikuwa anataka kurudisha majeshi kwa Hamisa, hivyo wakawa wanatumiana meseji na chating huku wakiahidiana kuoana. “Hata hivyo, hadi mwisho wa sakata hilo haikujulikana mara moja kama wamekubaliana kuoana au la. “Kwa kifupi, meseji na chating za Mondi na Hamisa ndizo zilileta balaa.

“Baada ya kuona maji yamekorogeka, ilibidi Tanasha amuombe Fahyma, akaongee na Hamisa ili amuachie mume wake bila kujua huyo Fahyma ndiye connector (muunganishaji). “Unaambiwa watu wanaoijua ishu kamili, ndiyo wakambana Fahyma kila kona huku wakimtaka kuacha dhambi ya usaliti kwa mtoto wa watu.

FAHYMA ABANWA

“Kwa hiyo ninyi kama mnataka ubuyu kamili mpigieni Fahyma mumuulize ukweli, maana nasikia alibanwa hadi kijasho chembamba kikamtoka na sijui kama ana ukaribu tena na Tanasha kama mwanzo,” kiliweka nukta chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina hadi masia atakaporudi.

MSIKIE FAHYMA

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Fahyma na baada ya kupatikana alisema kuwa, hata kama ni kweli yeye hawezi kueleza jambo lolote. “Unajua mimi siyo pikipiki Posta eeh? Halafu Diamond na Tanasha wanapendana jamani, hata kama wana matatizo ni yao wawili, mimi hawawezi kunitumia kama kipikipiki Posta kwa Hamisa.

“Kwanza, Tanasha hawezi kunituma, na mimi kufanya hivyo ni kitu ambacho hakiwezekani japokuwa ni kweli wote (Tanasha na Hamisa) ni rafiki zangu na mara nyingi nimekuwa nao sehemu mbalimbali. “Lakini siwezi kuwa kuwadi wa mapenzi yao, nitakuwa nakosea sana. “Kwa kifupi tu ni kwamba, Diamond na Tanasha hata kama wana matatizo, wanayamaliza wenyewe,” alisema fahyma ambaye kuna madai kuwa alifunga ndoa ya kimyakimya na Rayvanny.

TANASHA ANASEMAJE?

Katika maelezo yake juu ya ishu hiyo alipohojiwa, Tanasha hakupenda kuongea sana zaidi ya kusema tu kwa kifupi kwamba anamuamini mzazi mwenzake hivyo wanaojibebisha kwake waache mara moja. “Sijali kuhusu uhusiano wake uliopita, ninaangalia nilipo sasa. “Ninamuamini sana Diamond, kwa hiyo naomba hao wanaomfuatilia waache,” alisema

Wenye Video Chafu za Meninah Kimenuka!

 

HAKUNA aliye salama! Hiyo ndiyo taarifa kutoka Jeshi la Polisi ambayo imetua kwenye Dawati la Gazeti la Ijumaa Wikienda kwamba, wale wote ambao wamesambaziana video chafu za ngono zinazodaiwa ni za msanii wa Bongo Fleva na mshereheshaji Menina Atick ‘Meninah’, watafikiwa na mkono wa sheria.

GUMZO LILIIBUKA ALHAMISI

Video hizo zinazomuonesha Meninah akiwa anavunja amri ya sita na mwanaume ambaye haonekani sura, zilikuwa gumzo zaidi kwenye mitandao ya kijamii Alhamisi iliyopita ambapo watu mbalimbali walitoa maoni yao. Wengine walimponda Meninah, lakini wengine wapo waliomtetea.

CHANZO KUTOKA POLISI

Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Kinondoni, Dar, msako mkali wa kiuchunguzi utafanyika ili kuhakikisha wote waliohusika kusambaza picha hizo wanakamatwa na kufikishwa polisi kisha kufunguliwa mashtaka chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao.

“Yaani ni hatari, wapelelezi watawafikia watu wengi sana katika hii kesi maana Meninah amemshtaki mmoja wa wasambazaji wa picha hii, tayari amekamatwa. Sasa kama unavyojua ukifuatilia mlolongo wa watu kusambaziana hauishii kwa huyu mtu pekee aliyekwishakamatwa,” kilisema chanzo hicho.

CHAZIDI KUTIRIRIKA

Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, watu wote ambao wamesambaziana video hizo wanaweza kufikiwa kirahisi kwani teknolojia inawezesha wao kujua video hii imetumwa kutoka kwenye kifaa gani na kwenda kwenye kifaa cha nani.

“Ni rahisi tu sisi ku-track hadi kuupata mtandao wote. Hivi vifaa kama kompyuta, simu, ipad na vinginevyo, kinapokamatwa kifaa kimoja, kuna uwezekano polisi kuweza kutambua imesambazwa kwenda kwenye vifaa gani vingine pia ni rahisi kumjua mtumiaji wa hicho kifaa hususan katika simu ambapo zote zimesajiliwa,” kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya Jeshi la Polisi.

TAHADHARI YATOLEWA

Chanzo hicho ambacho pia ni miongoni mwa polisi, kilitumia nafasi hiyo pia kuwaasa Watanzania kuwa makini katika kipindi hiki ambacho Sheria ya Makosa ya Mtandao inafanya kazi kwani bila kujua, muda wowote unaweza kujikuta kwenye mikono ya sheria na una kesi ya kujibu.

“Wananchi wawe makini mno, hiki siyo kipindi kile cha watu kuona tu vitu na kurusha kwa marafiki. Ukiona mtu amekurushia kitu, usisambaze kabisa kwa watu wengine. Unaweza kukuta yule aliyekurushia amekamatwa na wewe ukajikuta umekamatwa vilevile,” alisema polisi huyo.

TUMSIKILIZE KAMANDA KINONDONI

Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Mussa Taibu ambapo alipopatikana alikiri kumshikilia mtu mmoja ambaye Meninah anamlalamikia kusambaza video zake chafu mitandaoni.

“Tupo naye polisi tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Kamanda Taibu bila kumtaja mtuhumiwa huyo wanayemshikilia. Hata hivyo, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa maofisa wa polisi anayehusika na Kitengo cha Makosa ya Kimtandao (Cyber Crime) wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambaye alimtaja mwigizaji mmoja Bongo ambaye alikuwa swaiba wa Meninah kuwa ndiye wanayemshikilia.

Wakati Gazeti la Ijumaa Wikienda linakwenda mitamboni, yaliibuka madai kuwa Menina amekamatwa na polisi kwa kosa la kusambaza video za lugha chafu kwa viongozi, lakini hata hivyo alipotafutwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema taarifa hizo hazijamfikia mezani kwake.

Mapya Yaibuka ! Tanasha Atibuliwa na Mobetto kwa Kufuma SMS zake Kwenye Simu ya Diamond

Tanasha, Hamissa Mobeto na fahyma

Kwa mujibu wa chanzo, hivi karibuni Baada ya Tanasha kujifungua walichuniana na Mond Baada ya Tanasha kudaiwa kufuma chats za Mobetto na Mond wakitaka kurudiana huku wakidaiwa kuahidiana kufunga ndoa. Fahyma ndie anadaiwa kuwa kuwadi wa Mobeto na Mond kwani Fahyma na Mobetto ni marafiki walioshibana kwa mujibu wa taarifa .

Fahyma pia ni rafiki wa karibu na Tanasha hivyo Tanasha alidaiwa kutofurahishwa na kumtaka Fahyma azungumze na Mobeto awe mbali na Diamond .

Fahyma alipoulizwa na gazeti la Risasi kuhusu issue hiyo amejibu .

“Unajua mimi siyo pikipiki Posta eeh? Halafu Diamond na Tanasha wanapendana jamani, hata kama wana matatizo ni yao wawili, mimi hawawezi kunitumia kama kipikipiki Posta kwa Hamisa. Kwanza, Tanasha hawezi kunituma, na mimi kufanya hivyo ni kitu ambacho hakiwezekani japokuwa ni kweli wote (Tanasha na Hamisa) ni rafiki zangu na mara nyingi nimekuwa nao sehemu mbalimbali. Lakini siwezi kuwa kuwadi wa mapenzi yao, nitakuwa nakosea sana. Kwa kifupi tu ni kwamba, Diamond na Tanasha hata kama wana matatizo, wanayamaliza wenyewe,” alisema fahyma .

Kwa upande wa Tanasha alipoulizwa na Risasi amesema

. “Sijali kuhusu uhusiano wake uliopita, ninaangalia nilipo sasa. Ninamuamini sana Diamond, kwa hiyo naomba hao wanaomfuatilia waache”

Majibu ya Fid Q kuhusu picha yake na Nandy

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Mkongwe wa muziki wa HipHop Bongo Fid Q, amenyoosha maelezo kuhusu picha iliyosambaa na kuzua taharuki katika mitandao ya kijamii ikimuonesha amesimama na Nandy.

“Kwanza yale yalikuwa mambo ya upepo, nilishangaa kwa sababu mambo ya walimwengu niliipokea kama ya walimwengu kwahiyo sio ‘issue’, Mke wangu Mama Cheusi hakutoa maoni yoyote kuhusiana na ile picha ni kama hajaiona bado” amesema Fid Q.

Pia msanii huyo ameongelea suala la watu wengi kutegemea sana mitandao ya kijamii kama kuzusha habari, kupata umbea au kufuatilia maisha ya mtu.

“Ni hatua ambayo ilibidi tufike lakini wasiwasi wangu ni mapokeo ya wengi yamekuwa si sawa sana kwa sababu wengi wanatumia huko kuwaumiza watu kwa kusemwa , kutukanwa , kusimangwa ndiyo maendeleo hayo yanakuja hivyo mengine kwa njia ya hasi mengine kwa njia ya chanya kwa sisi wasanii, tunaichukulia kama sehemu ya kujitangaza na zaidi imetupa nguvu ya kujiwezesha kama kutokuwa watumwa wa vyombo vya habari” ameongeza.

Aidha amesema kuna tofauti kati ya maisha yake binafsi ambayo ni siri na yale ambayo yapo mbele za watu.