Huwezi Amini Huyu ni Mwanaume Shoga Tajiri Huko Nigeria, Anaitwa Bobrisky

Shoga maarufu kutoka pande za +234 , Idris okuneye(28), maarufu kama BOBRISKY, ndiye staa shoga aliyeamua kujiweka wazi nchini Kwao kwa kuvaa na kuishi kama mwanamke, unaambiwa hutumia mamillion ya pesa kujiremba na ku maintain muonekano wa kike.

Shoga huyo ambaye pia ni rafiki wa muigizaji mkongwe, Tontoh Dikeh, amekua akivutia watu mbali mbali kwa umahiri wake wa kujiremba na kuishi maisha expensive pengine kuliko mastaa wengine nchini humo.

Bobrisky anajihusisha na biashara ya vipodozi ambayo anadai ndo iliyompa utajir wa kutisha mpaka sasa, ingawa hata yeye mwenyewe pia amewahi kusema mara kwa mara kuwa anatoka na ma politician na watu wazito wenye pesa zao nchini humo ambao pia wanampa jeuri ya kuishi maisha ya kifahari huko Lagos state


Muonekano wa zamani kabla hajabadili muonekano wake

Usikubali Kuogopa Kumuonyesha Mke au Girlfriend Wako Unampenda Kisa Unaogopa Washkaji Watakuona Bwege

Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda kisa unaogopa washkaji au ndugu watakusema umekaliwa naye.

Ni tabia mbaya sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti “mimi bwana mwanamke hawezi niuliza niko wapi” sasa ndugu yangu wewe ndio ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic.

Tusifanye vitu ili kuwaridhisha washkaji huko viringeni…tufanye vitu kuwaridhisha wake zetu…. imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa saba usiku unaonekana bwege na ukiangalia ligi ya ulaya sebleni kwako na mke wako unaonekana bwege pia…au usipokua na demu wa nje eti wewe sio mjanja. huu ni upuuzu tubadilikeni jamani. ndio sikatai usikae na washkaji lakini usipitilize sasa.

Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likuuubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia..jamani ?

Hizi Ndio Aina Tatu za Michepuko Hapa Bongo1. Mchepuko wa Lami: huu ni ule ambao
hauombi pesa, upo njema unajua designer
zote, katulia hana mapepe, uwe nae usiwe
nae maisha yake yanaendelea.

2. Mchepuko wa Vumbi: huu ni ule ooh sina
pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa,
charge iko low, ooh nipo saloon nadaiwa elfu
thelathini nitumie kwa tigopesa, naomba
nauli, nadaiwa kodi, mtoto wa shangazi kaja,
nrushie dompo, nk. Na hii ndio noma maana
njia kuu lazima washtukie mchepuko vumbi
unachafua na unasumbua fulltime!

3. Mchepuko kokoto: huu ni mkali zaidi ya
njia kuu kila mara huuliza upo wapi? na nani?
Why hupokei simu yangu? Nomaaaa!
Baki njia Kuu!

Q CHILLA ‘AOTA’ KURUDIA ENZI

MWANAMUZIKI wa Kizazi Kipya, Abubakary Katwila ‘Q-Chillah’ amejitapa kurudi katika gemu la muziki kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipokuwa akitamba na ngoma mbalimbali ikiwemo Si Ulinikataa ambayo ilidaiwa kuwa ni historia ya kweli ya maisha yake.  Akizungumza na Risasi Vibes, kwenye Klabu ya Forty Forty iliyopo Tabata-Bima Dar, Q-Chillah anayetikisa na Ngoma ya Tikisa aliyoiachia hivi karibuni alisema kuwa itamtasaidia kumrudisha enzi zile alipokuwa gumzo na ngoma zake mbalimbali ikiwemo Si ulinikataa, Kosa langu na nyinginezo.

“Ndugu mwandishi kuna hii Tikisa na ngoma zangu zingine ambazo ziko jikoni zikishakamilika nakukuhakikishia ni lazima zinirudishe kwenye enzi zangu. “Kuna kipindi nilipotezwa na vishawishi na kuingia kwenye mambo yasiyofaa ambayo yalitaka kuniangamiza lakini sasa nimeshajitambua na ninachodili nacho ni kupiga kazi kwa juhudi maarifa. “Kama nilikuwa juu kwa juhudi zangu siwezi kushindwa kurudi tena baada ya kukaa na kutafakari nilipokosea na kugundua makosa yangu.”

KALA JEREMIAH ALIVYOPATA TABU KUFUGA ‘MWEMBE’ HUU – VIDEO

RAPA Kala Jeremiah ambaye hivi karibuni ameachia ngoma zake mbili #NISAMEHE na #AMERICA, amefunguka na kusema kuwa alipata wakati mgumu kubadilisha mwonekano wake ikiwemo kufuga nywele na kidevu kama ‘Osama’ ili kutengeneza uhalisia wa ujumbe aliotaka kuufikisha kwa jamii.

Amesema nyimbo hizo zina uhalisia wa maisha ya kawaida wanayokutana nayo watu wengi ikiwemo unyanyasaji wa wanawake na vijana kuamini kuwa kutoboa maisha ni kwenda Ulaya au Marekani, lakini hata hapahapa nyumbani Tanzania kuna fursa kibao ambazo wanaweza kufanya na wakatoboa.

LULU DIVA AMFUNGUKIA RIYAMA

STAA wa Bongo Fleva ambaye, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amemfungukia staa mwenzake kwenye tasnia ya filamu Bongo, Riyama Ally kuwa anajua kuvaa uhalisia hadi kero.

 

Akipiga stori mbili tatu na Za Motomoto, Lulu Diva alisema kuwa, kama unaigiza muvi moja na Riyama halafu uwe na chongo kwenye filamu, anaweza kulichamba hilo chongo lako hadi ukashindwa kujibu chochote.

 

“Yule dada anakuchamba kama anachamba kweli, unaweza kumuomba msamaha kwenye muvi. Akimaliza kushuti unaweza kumfuata na kumuuliza dada pale ulikuwa unamaanisha au?” alisema Lulu Diva

MAJIBU YA AUNT KUHUSU IYOBO: NIFE NA MAJANGA YA KUVUMILIA KISA INSTAGRAM?


MSANII wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ameamua kufunguka na kuweka wazi kuhusu wanaomsema kufuatia kuachana na mzazi mwenzake, Mose Iyobo.

Kupitia ukurasa wake a Instagram, Aunt ameandika waraka mzito kuhusu sakata hilo huku akiwatolea povu ile mbaya watu wanaomtukana mitandaoni kutokana na uamuzi wake wa kuachana na Iyobo na kuchukua mwanamme mwingine.

Habari zenu? Naitwa Aunty Ezekiel (Mama Cookie), nimeona niaongee hili ili kuwa nafasi ya kila mmoja muendelee na kazi zenu maana naona leo kuna wengine mmeacha yenu kabisa kama kawaida wajuzi watoa nasaha Washauri wa Instargam, mnaojua maisha kushinda mtu yoyote yule, mnaojua kuna kudharirika kushinda wenye maisha yao.


Bana natamani mjue tuu labda kama kuna wageni humu kwa wenyeji naomba mfahamu mimi sifundishwi maisha plz plz plz, endeleeni na yenu msinifundishe cha kufanya, najidharirisha kuwa na bwana mwingine mnataka nipige Puchu?

Bwana angu niliyenaye shoga alilala na baba akoo! Halafu naomba ikumbukwe haya ni Maisha yangu Mm na Familia yangu sio ya kwenu.


Hata hayo Mnayoyaona now mliyapenda ni mimi ndio nilifanya myapende, mlianza hivyo hivyo, so plz naomba tu niwakumbushe THIS IS MY LIFE. Na hayo mnayotamani niyaongee sitakaa niongee, kwa taarifa yenu mimi nimefundwa sijatoka juu ya miti, nimelelewa siwezi muongelea mtu aliyenipeleka labour hata iweje.

Maana haya majina hayawezi kubadilika, tutabadilika sisi na mahusiano yetu, sio hili jina la huyu mtoto plz… msipende kugombanisha watu nyie hamtaki watu waachane kama nani khe! Tufe na majanga ya kuvumiliana ndani kisa Instagram watanionaje?


Huo  upuuzi sijafanya, bado naishi maisha yangu nitakayo sio mtakayo nyinyi, nina maisha yangu, ana maisha yake hayo ni makubaliano yetu nyinyi yanawahusu nini?

Looh! hebu plz bana, mnataka watu hadi siku wasisalimiane ndio huwa mnaona utamu! PUMBAVU, hebu naomba mniache plz…. Nina mtoto anaejua kuchezea simu na siku moja atakuwa atayakuta, mnataka anichukulie vipi?


Naomba mniache na haya yote nafanya course of My Baby Girl na sio mwingine yeyote. Msije mkajipa imani eti nitaona haya oooh mara kujidharirisha, mama zenu wabadili mabwana sisi tukibadili tunajidharirishaa, Aaah kina mwajuma vipi babuuu.

Hebu tufunge huu mjadala mnalotaka hamtalipata kwangu, endelea ku-enjoy na picha kutoka nyanda za juu kabisa nikiwa na haka kamarioo au kashoga toka Zanzibar, kwangu mimi ka-handsome boy, nite nite, mtazoeatuu!

MSAIDIZI WAKE AFICHUA SIRI NZITO YA MARIAH CAREY

MWANAMUZIKI Mariah Carey ana makalio ya bandia, hii imethibitishwa na aliyekuwa msaidizi wake Lianna Shakhnazarryan kwenye mgogoro wao wa kisheria unaoendelea.

Imeelezwa kua, baada ya Carey kumburuza mahakamani Lianna kwa madai ya kumtishia kuvujisha picha zake chafu, Lianna naye alimfikisha mahakamani Careyakidai kuwa ni wizi wa fedha uliofanyika kwenye akaunti yake ya benki ambapo Carey alichukua pesa na kwenda kufanyia upasuaji wa makalio yaani Plastic Surgery.

Kwa mujibu wa Daily MailLianna ameieleza mahakama kwamba Maria alichukua Card yake ya benki na kwenda kutoa pesa akitumia jina la (Stella Carey) na kuchota kiasi cha dola 10,000 kwa kwa ajili ya upasuaji huo, pia alikomba dola 4,800 kwa ajili ya kunenepesha matiti na dola 8,900 kwa ajili ya kutengeneza shingo yake na sehemu za taya.

KAJALA AFICHUA CHIMBO JIPYA LA MASTAA!

STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja amefichua chimbo jipya la mastaa lililopo katika msitu wa Magoroto uliopo Wilaya ya Muheza, kilomita 37 toka katika Jiji la Tanga.  Akizungumza na gazeti hili la Risasi Mchanganyiko, Kajala alisema amekuwa akienda eneo hilo kwa ajili ya kupumzika na kula bata, akashangazwa na mandhari yake ambapo inaelezwa kuwa mastaa kibao wamekuwa wakifika.

“Jamani sasa hivi ni ngumu sana kuona mastaa wanaopenda sehemu tulivu wamekwenda kujiachia kwenye viwanja vya Dar, wengi sasa hivi wanaenda Magoroto, aisee kuna raha. “Kule hata uwe na msongo wa mawazo kiasi gani yanapotea fasta kwa kuwa ni sehemu tulivu mno na mara nyingi siku za mwisho wa wiki naenda kwa ajili ya kupoteza mawazo na kuangalia uzuri wa nchi yangu,” alisema Kajala.

Staa huyo aliongeza kuwa watu wengi ambao ni maarufu wanapenda kwenda kupumzika eneo hilo kwa sababu kuna vitu vingi vya asili kama milima, kijani kibichi, ndege na hali ya hewa safi. “Mimi kuna wakati nilitamani nitafute nyumba maeneo ya kule ili kila wikiendi iwe rahisi kwenda kujiachia, yaani ukijaribu kwenda mara moja utatamani iwe hivyo mara kwa mara,” alisema Kajala.

Baadhi ya mastaa ambao wametajwa kutinga katika chimbo hilo siku za hivi karibuni ni Diamond Platnumz ambaye licha ya kuwahi kutengeneza video katika eneo hilo amekuwa pia akipendelea kufika, DJ Sinyorita, Maua Sama, Ben Pol na wengineo.

Undani kuhusu Marogoto Msitu wa Magoroto uliopo Wilaya ya Muheza una ukubwa wa ekari 591 na ziwa la maji masafi na unatengeneza vipande vya milima ya Usambara ambayo inafahamika kwa uzuri na upekee wa uoto wa asili.

Msitu huo unafahamika zaidi kwa uwepo wa ndege wa kipekee ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Chama cha Uhifadhi Wanyamapori wanahusika katika uhifadhi wa misitu hiyo nchini. Mogoroto ni kivutio cha utalii siyo Muheza pekee bali kwa mtu yoyote mwenye nia ya kutembelea eneo hilo kutokana na hali yake ya hewa kuwa nzuri huku ikiambatana na mandhari nzuri ya chini ya milima.

NAMUONA LULU NDANI YA JENNIFER KANUMBA

KWA wafuatiliaji wa filamu tangu enzi zile ambazo filamu ilikuwa filamu kwelikweli, watakuwa wanamkumbuka vizuri binti mdogo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Hanifa Daudi ‘Jennifer Kanumba’. Huyu ni mmoja wa wasanii walioibuliwa na marehemu Steven Kanumba ambapo alikuwa akimtumia kwenye filamu zake mbalimbali akiwa na mwenzake wa kiume anayefahamika kwa jina la Patrick. 

 

Patrick na Jennifer walikuwa ‘mapacha’ ambao ilikuwa wakiigiza filamu na Kanumba ni lazima ibambe. Hii ilitokana na vipaji walivyokuwa navyo watoto hawa.

 

Walikuwa watundu, wabunifu na waliokuwa wakijua kujiongeza wanapokuwa mbele ya kamera. Kutokana na uwezo wao huo, wengi waliwatabiria makubwa. Jennifer na Patrick walionekana kuja kuwa mastaa wa baadaye na hakika Jennifer alikuwa akipita mulemule alimopita staa mkubwa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Kwa wasiofahamu Lulu alianza kuigiza akiwa na umri mdogo sana. Akaonesha uwezo mkubwa hadi leo hii ukiwataja wasanii wanaofanya vizuri kwenye uigizaji Bongo, Lulu hawezi kukosekana. Ndivyo ilivyokuwa ikionekana kwa Jennifer. Bahati mbaya sana ni kwamba, mtu aliyekuwa akiwaongoza kuelekea kwenye mafanikio Mungu aliamua kumchukua.

 

Hapa namzungumzia Kanumba The Great ambaye ndiye aliyewaibua watoto hao, akawashirikisha kwenye filamu zake kama vile This Is It, Big Daddy, Uncle JJ na nyinginezo ambapo kila aliyewatazama watoto aliona kitu kikubwa ndani yao. Bahati nzuri hata wenyewe walipokuwa wakihojiwa walieleza ndoto zao za kuja kuwa waigizaji wakubwa Bongo. Ndoto zao zikazimika baada ya Kanumba kufariki dunia.

 

Nakumbuka wakati Kanumba anafariki, watoto hawa walilia sana. Ilikuwa ni kama wameondokewa na mzazi ama mlezi wao. Yawezekana walikuwa wakililia mengi lakini naamini kubwa lililowaliza ni kwamba nguzo yao waliyokuwa wakiitegemea kwenye sanaa ilikuwa imeanguka. Na kweli, baada ya kifo chake sikuwasikia tena watoto hao. Nilitarajia kuona wasanii waliobaki wakiendeleza vipaji vyao lakini hakuna aliyechukua nafasi ya Kanumba.

Matokeo yake watoto hawa wakapotea. Mara kadhaa walipokuwa wakiulizwa kwa nini wameikacha sanaa walikuwa wakisema kuwa, wameamua kukomalia masomo kwanza, mambo ya sanaa yatafuata baadaye. Yalikuwa ni majibu sahihi lakini ukweli ulibaki palepale kwamba, hawakuwa na mtu wa kuwashika mkono.

 

Kwani enzi wanaigiza na Kanumba hawakuwa wanasoma? Jibu ni Hapana! Lakini pia mbona Lulu alikuwa akiigiza huku akiwa anaendelea na masomo? Mbona wapo wasanii wengi tu ambao licha ya kwamba walikuwa wakisoma lakini waliendelea kufanya sanaa? Maswali hayo yanatufanya mimi na wewe tuhitimishe tu kwamba, kilichowafanya watoto hawa wapotee ni kukosa sapoti kama waliyokuwa wakiipata kutoka kwa Kanumba.

 

Miaka kadhaa imepita sasa, namuona Jennifer ni kama anataka kurudi tena kwenye game. Nimekuwa nikimfuatilia sana kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye ukurasa wake wa Instagram. Anaonekana ni binti anayewiwa kurudi kwenye sanaa. Swali ni je, nani anayeweza kumshika mkono ili kumuendeleza pale Kanumba alipokomea?

Ukifuatilia kwenye ukurasa wake wa Insta utaona kila siku anaposti picha za mapozi mbalimbali kama wanavyofanya akina Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jack Wolper na wengineo. Amekuwa mkubwa, amekuwa mzuri, mrembo na anayejitambua kiasi kwamba ukichanganya na kipaji chake anaweza kufaa sana kwenye hizi tamthiliya na filamu zetu. Hakika namuona Lulu mpya kwa binti huyu.

 

Sijui kwa nini nina imani hiyo lakini niweke wazi tu kwamba, mimi nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa kazi za sanaa za binti huyu tangu enzi zile. Najua uwezo wake, najua anaweza! Swali ni je, bado ana ‘interesti’ ya kuigiza? Je, hali ya soko la filamu kwa sasa inaweza kumfanya aogope kukitumia kipaji chake?

 

Je, anaweza kuiamini filamu kuwa inaweza kuyabadili maisha yake au ana ndoto nyingine baada ya kumaliza shule? Kwa sasa sina majibu ya maswali hayo lakini nikipata bahati ya kuongea naye nitakuwa na lingine la kuzungumza.