KAJALA: KUTEKETEZA MILIONI KWA MTOKO KAWAIDA SANA!

Nsiku nyingine tena tunakutana katika safu hii ya My Style ambayo inazungumzia mastaa mbalimbali na kueleza maisha yao ya kila siku yanavyoenda.

Leo tunaye staa mwenye viwango vyake kutoka Bongo Muvi, Kajala Masanja ambaye pia anamiliki kampuni yake ya filamu, Kay Entertainment. Hadi sasa ameshacheza filamu nyingi ambazo zimempa chati mbalimbali kama Devil Kingdom ya KanumbaSikituFundi SeremalaLaanaPishu na Mbwa Mwitu.

Katika safu yetu hii, Kajala ataweka wazi style yake ya maisha ya kila siku kuanzia mtoko hadi manukato kama alivyokuwa akihojiana na My Style.

My Style: Msomaji angependa kufahamu kwanza ni kitu gani unapenda kwenye maisha yako ya kila siku?

Kajala: Napenda sana kutuliza akili yangu wakati wote, napenda kukaa sehemu ambayo haina vurugu kwa sababu mimi mwenyewe sipendi kabisa purukushani na mtu yeyote yule.

My Style: Marafiki zako ni wa aina gani au unapenda wawe na tabia gani?

Kajala: Kwanza kabisa mimi kama Kajala huwa sina urafiki wa ndani kabisa kama ilivyo kwa wengine ila napenda tu kampani ya kawaida tukimaliza kila mtu ana zake lakini pia napenda kuzungukwa na watu wanaojielewa, wanaoweza kunifanya nikacheka kila wakati.

My Style: Una muda wa kukaa jikoni na kupika?

Kajala: Ninaweza lakini nina msaidizi ambaye anafanya hivyo kwa sababu ya kazi zangu za kila siku lakini kama naingia jikoni natoa kitu kizuri.

My Style: Vipi kuhusu upande wa kutoka unaweza ukatupia mwilini kama shilingi ngapi?

Kajala: Kwa kweli napenda sana kupendeza, wakati wowote hivyo kama mtoko ule ambao nimeupangilia kumaliza milioni ni kitu kidogo kuanzia begi, nguo na nywele.

My Style: Unatumia manukato gani, maana watu wengi wanasema unanukiaga sana.

Kajala: Nachanganya sana sana! Ila nikitoka siwezi kukosa kujipulizia Olympia, Tom Ford, Jadore na Scandal yaani nachanganya napata harufu nzuri sana.

My Style: Vipi maisha yako wewe na Paula?

Kajala: Ni marafiki sana, lakini kuna wakati navaa umama nakuwa mbogo mwisho wa siku kila mmoja akikaa mbali na mwe-nzake tuna-kumbu-kana.

My Style: Unapenda kufanya mazoezi na unapendelea kufanya muda gani?

Kajala: Mazoezi ni kitu ambacho naweza kusema kipo kwenye damu yangu. Napendelea sana kwenda kufanya asubuhi maana nikimaliza nafanya mambo yangu jioni kama siku za wikiendi.

My Style: Unapendelea wageni wa aina gani nyumbani kwako?

Kajala: Mgeni yeyote napenda ila awe mstarabu tu maana kwangu naona kama mgeni ni Baraka.

My Style: Nguo mpya huwa unanunua baada ya muda gani?

Kajala: Kwanza kurudia nguo inakuwa shida yaani naweza kuvaa nguo mwaka huu na nikarudia mwaka ujayo.

My Style: Unaweza kuku-mbuka pochi zako za kubeba ziko ngapi?

Kajala: Nina pochi zaidi ya 30 na zote mara nyingi nanunua kua-nzia shilingi 70,000, 80,000 mpaka 100,000.

My Style: Vipi kuhusu mapenzi yana nafasi gani kwenye maisha yako?

Kajala: Nafasi yake kwangu ni ndogo sana maana sasa hivi niko mbio kuhu-siana na maisha yangu.

My Style: Unakumbuka Mara ya mwisho kwenda Kanisani lini?

Kajala: (Kicheko) Niliwahi kwenda mwaka jana lakini sasa hivi nitaanza kwenda kanisani tena maana ni jambo jema kumshukuru Mungu.

My Style: Haya nashu-kuru kwa ushiri-kiano wako.

Kajala: Asante sana karibu.

NANDY APINDUA MEZA MDOGOMDOGO

FEBRUARI 9, 2017 bado itaendelea kubaki kama kumbukumbu katika kichwa cha mwanadada mrembo anayetikisa Bongo Flevani, Faustina Charles Mfinanga anayetumia majina ya Nandy au The African Princess anapokuwa stejini. Hiyo ndiyo siku iliyofungua rasmi safari yake ya muziki baada ya kuwa mshindi wa pili katika mashindano ya kuimba ya Tecno Own the Stage yaliyofanyika nchini Nigeria na kujizolea kitita cha zaidi ya shilingi milioni 35 za Kibongo.  Baada ya kuianzisha safari hiyo ni kama gari lililowekwa mafuta full tank kwani amekuwa akifanya poa na kutingisha tasnia ya muziki Afrika Mashariki kiasi cha kubatizwa majina mengi kama vile Sauti ya Asali na The African Princess. Leo hii Nandy yule aliyezaliwa 1992 kule Moshi mkoani Kilimanjaro, aliyekuwa akipiga shoo na B Band chini ya Banana Zorro miaka ya 2010 si yule tena.

Kuna utofauti mkubwa wa Nandy yule aliyekuwa Jumba la Kuibua Vipaji Tanzania (THT) kipindi hicho akiwa na ngoma ya kawaida sana ya Bye (My Ex). Over Ze Weekend limekuandalia baadhi tu ya vitu ambavyo vimemfanya Nandy kuwa juu na wa tofauti ambapo wasanii wengi wa kike wameshindwa kupitia nyayo hizo hivyo kupanga foleni nyuma yake.

KUMILIKI STUDIO

Ni moja ya mafanikio makubwa kwa Nandy ambapo asilimia kubwa ya nyimbo zake anazipikia katika studio yake aliyoiita African Princess. Bidada huyu anasema lengo hasa la kumiliki studio nyumbani kwake ni kurahisisha muziki wake.

“Siyo kama studio za watu wanakaa foleni nje, hapana hii kwa ajili yangu na wale nitakaokuwa ninawashikirikisha kwenye nyimbo zangu. Lakini pia kwa hapo baadaye tutaangalia utaratibu wa wasanii wengine,” anasema Nandy. Studio hiyo kwa sasa inasimamiwa na Prodyuza Kimambo.

ALBAM

Hadi sasa Nandy anamiliki albam moja inayokwenda kwa jina la African Princess ikiwa na nyimbo 13 ambazo miongoni mwake ni One Day, Wasikudanganye, Kivuruge, Subalkheri, Njiwa, Aibu, Ninogeshe na Nagusagusa. Albam hii aliizindua rasmi usiku wa Novemba 9, 2018 na kuwa msanii wa pili wa kike kuzindua albam akiwa nyuma ya Vanessa Mdee ‘Vee-Money’ ambaye aliizindua albam yake ya Money Mondays.

MFANYA-BIASHARA

Kitu kingine kinachomfanya kuendelea kuwa juu ni kutokana na kujihusisha katika biashara ambapo kwa sasa anamiliki kampuni ya kutengeneza nguo ya Nandi African Prints na Nandy Beauty Products ambayo ameingia ubia na kampuni ya vipodozi ya Grace akiingiza matolea mawili ya Nandy Beauty Soap na Nandy Petroleum Jelly.

TUZO

Nandy anashikilia tuzo kadhaa ambazo ni Marantha na Dear za nchini Kenya kupitia Cover aliyofanya kwenye wimbo wa Injili wa msanii Angel Benard wa Nikumbushe Wema Wako. Tuzo nyingine kubwa ni ya AFRIMMA ambayo aliipata mwaka 2017 katika kipe-ngele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mash-ariki.

TAMT-HILIA YUMO

Licha ya kutikisa kote huko, Nandy bado ameonesha kipaji chake katika uigizaji ambapo kwa sasa anashiriki Tamthiliya ya Huba inayorushwa na Maisha Magic Bongo kupitia King’amuzi cha Dstv.

TAMASHA

Ameonesha ukomavu kwenye gemu ndani ya muda mfupi baada ya kuandaa tamasha lake mwenyewe aliloliita Nandy Festival ambalo lilifanyika Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Mpira wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga.

Katika usiku huo, Nandy alikuwa msanii wa kike aliyeshindana na wasanii wengine waliokuwa wakifanya shoo za viwanjani ambao ni Diamond Platnumz aliyefanya Uwanja wa Mpira wa Kahama na Harmonize aliyefanya Uwanja wa Mpira wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Huyo ndiye Nandy ambaye anapindua meza mdogomdogo akiwapangua wakongwe wa kike mmoja baada ya mwingine!

VIDEO MPYA DJ DAVIZO FT. CHIN BEES, ITAZAME HAPA

DUDE jipya linalotikisa kwa sasa mtaani, kwenye Stations mbalimbali za Radio na Televisehni Bongo na nje ya nchi ni video ya mkali wa Bongo Fleva, DJ Davizo, wanapenda kumuita Selekta Davizo.

DJ Davizo ambaye amewahi kufanya ngoma ya SUKUMA na Barakah The PrinceINAMA aliyofanya na Chin Bees, ameachia tena video mpya Mei 22, mwaka huu inayoitwa CHAMPION ambayo amemshirikisha Rapa mwenye vurugu na mapafu ya mbwa akiwa stejini Chin Bees.

Champion imetengenzwa na Producer Goncher Beatz katika Studio za Wanene Entertainment.

KUMBE AUNT NA IYOBO MAMBO POA TU!

Mwanamama wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel amesema kuwa pamoja na kwamba hayupo tena kimapenzi na mzazi mwenzake, Mose Iyobo ‘Moze’ lakini ukweli ni kwamba wako poa tu na wanasalimiana kama kawa. Aunt aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kugombana kwao kwenye masuala ya kimapenzi hakuwezi kuathiri malezi ya mtoto wao, Cookie kwa vile wao ni wazazi na wana haki ya kuzungumza chochote.

Kuna watu wanajua mimi na Iyobo hata tukionana hatusalimiani, siyo kweli, Yule ni baba wa mtoto wangu hivyo tunazungumza na tunacheka panapostahili,” alisema Aunt ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na Iyobo aitwaye Cookie.

ENZI ZA UTOTONI, UNAAMBIWA KAJALA ALIKUWA HAOGI

Ukiona mastaa Bongo sasa hivi wanajipenda na kupendeza ni vigumu kujua huko nyuma walikuwa wengine hata wanarudi nguo siku nzima.

Sikia hii ya mwigizaji mahiri wa Bongo Muvi, Kajala Masanja ambaye ukimuona sasa hivi ni mwanamke anayejipenda na kunukia kila wakati, lakini huko nyuma unaambiwa ilikuwa mbinde kuoga.

Akizungumza na Imefunuka ya Ijumaa Wikienda, Kajala alisema kuwa alipokuwa kidato cha kwanza ambapo alianzia shule moja mkoani Songea, kulikuwa na baridi kali kiasi kwamba alikuwa akiamshwa asubuhi kwenda kuoga, akifika bafuni, anakaa kama nusu saa halafu anamwaga maji chini kisha ananawa uso na kutoka.

“Mimi na baridi ilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa kwa sababu ilikuwa tukiamshwa asubuhi kwenda kuoga, nacheza mchezo tu, nakaa kwa muda kisha namwaga maji chini. Nilikuwa naweza kupiga hivyo hata wiki nzima labda siku tupate moto tuchemshe maji ndiyo nilikuwa ninaoga,” alisema Kajala.

BINTI KIBOKO YA ZARI KUTUA BONGO

NYOTA ya binti wa miaka 18, Regina Daniels maarufu kama ‘Kiboko ya Zari’ raia wa Nigeria inazidi kung’aa baada ya kuwepo kwa mpango wa kumleta Bongo, Risasi Jumamosi limewekwa wazi. 

 

Mpango huo unasimamiwa na muongozaji filamu maarufu nchini, William Mtitu ambaye ameliambia Risasi Jumamosi hivi karibuni kuwa michakato ya kukamilisha zoezi hilo unaendelea.

“Baada ya habari zake kutoka, nilivutiwa naye, nimemfuatilia binti huyo na kujiridhisha kuwa ni mtu maarufu na ana uwezo mzuri wa kuigiza filamu.

“Kuhusu utajiri wake mimi sikuangalia sana hilo, nilichoangalia ni namna gani naweza kumleta hapa nchini na kufanya naye kazi kama ilivyokuwa kwa Omotola (Omotola Jalade Ekeinde, msanii wa kike kutoka Nigeria) miaka ya nyuma,” alisema Mtitu.

MPANGO WASUKWA

Mtitu aliongeza kuwa amejaribu mara kadhaa kuwasiliana na binti huyo moja kwa moja ili kujua upatikanaji wake pamoja na gharama zake ameshindwa na kwamba sasa anatafuta mtu wa kumsaidia kufanikisha mpango wake huo.

Alisema: “Kuna tamthilia naisimamia inaitwa Rebecca inarushwa kwenye king’amuzi cha DSTV ni nzuri na ina mashabiki wengi sana. “Nimeona ili kuiongezea chumvi nimlete Regina tushirikiane naye,” alisema Mtitu.

REGINA NI NANI?

Kwa mujibu wa nyanzo mbalimbali mitandaoni, Regina ni binti wa Kinigeria ambaye alianza kazi ya uigizaji akiwa na umri wa miaka 6 na alipofikisha miaka 18, aliolewa na mfanyabiashara bilionea aitwaye Ned Nwoko ’59’.

Ndoa yake na bilionea huyo inatajwa kuwa imemfanya binti huyo mrembo kuogelea kwenye maisha ya anasa ambapo mbali na kuishi kwenye jumba la kifahari na kumiliki magari ya bei mbaya, anayo pia ndege yake binafsi.

AFANANISHWA NA ZARI

Kutokana na aina ya maisha yake wengi waliopata habari zake walimfananisha na Zari ambapo alibatizwa jina mitandaoni kuwa ni ‘Kiboko ya Zari’ kutokana na kile kilichotajwa kuwa amemzidi uwezo wa kifedha.

FILAMU ALIZOCHEZA

Kwa mujibu wa mitandao, Regina anatajwa kucheza filamu mbalimbali nchini Nigeria kama Dumebi in School, Python Girl, The Bat-Man na The Jericho.

Nyingine ni Plantain Girl, Jaja the Great, Tears of Ojiugo, Wipe your Sorrows na Royal Covenant ambazo zote alifanya vizuri.

MPANGO WA MTITU UTAFANIKIWA?

Katika mazungumzo na muongozaji wa filamu Mtitu, mwandishi wetu alijaribu kutia shaka juu ya nia ya muongozaji huyo kumleta Regina nchini kufanikiwa ambapo mwenyewe alisema:

“Hakuna kinachoshindikana, sitakuwa peke yangu katika hili nitawashirikisha na wasanii wenzangu kufanikisha hili. “Marehemu Steven Kanumba alifanikiwa kufanya kazi na wasanii wa Nigeria, kwetu sisi hiyo ni njia ambayo ametutobolea mwenzetu, tunatakiwa kuifuata,” alisema Mtitu.

HISTORIA KUJIRUDIA

Endapo Mtitu atafanikiwa kumleta binti huyo Bongo haitakuwa jambo geni kwani wasanii wengi wa Nigeria na Ghana wameshawahi kuja nchini na kufanya sanaa na baadhi ya mastaa wa filamu wa Kibongo. Wasanii nguli waliowahi kuja nchini na kushirikiana kikazi na wasanii wa filamu Bongo ni Omotola, Van Vicker, Emmanuel Francis, Mercy Johnson, Ramsey Nouah na wengine wengi.

TIMU ZARI WAHAHA

Tangu habari za Regina zivume na kupewa jina la Kiboko ya Zari, Timu Zari imekuwa ikihaha mitandaoni kumponda binti huyo kwa kusema hana alichompita Zari. “Kampita kwa hizo hela za mumewe, ujinga mtupu.” “Wanampa sifa za kijinga kumkuza kichwa mwisho kiwe kikubwa kama cha tembo.” “Zari atabaki kuwa juu halinganishwi na wanuka jasho.”

Baadhi ya komenti mitandaoni zikionesha kuwa Timu Zari haikubaliani na mtazamo wa Regina kumzidi uwezo wa kifedha. Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa mijadala hiyo imekuwa ikizidi kumpaisha chati binti huyo ambapo habari zake kwenye mitandao ya kijamii zimekuwa zikifuatiliwa sana na watu.

UCHEBE AFUNGUKA KUMDUNDA SHILOLE

MUME wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ Ashiraf Uchebe, amesema tangu aanze kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo mpaka anamuoa hajawahi kumpiga hata kofi.

Uchebe ameibuka na maelezo hayo baada ya kuwepo kwa madai ya muda mrefu mitandaoni kuwa amekuwa na kawaida ya kumwangushia kipondo mkewe huyo.

Akizungumza na MIKITO Uchebe alisema watu wengi wanamuona kama baunsa ambaye kila wakati anaweza kupiga mtu, kitu ambacho si kweli kwani anampenda sana mkewe huyo na kamwe hawezi kumgu

“Watu wengi wananichukulia tofauti sana wananiona kama mtu wa kupiga kila wakati lakini siyo kweli kabisa, sijawahi kumpiga mke wangu hata mara moja na sitaweza kufanya hivyo,” alisema Uchebe.

Kwa upande wa Shilole, alipoulizwa kuhusu maelezo hayo, alisema ni kweli, tangu aolewe na Uchebe hajawahi kumgusa. “Sijui wanamuonaje mume wangu au kwa sababu kajazia ndiyo maana wanasema ananipigaga, yaani kiufupi hajawahi kunigusa kabisa,” alisema Shilole.

HUSNA MAULID: UYATIMA UMENIFUNDISHA MAISHA

MREMBOambaye amewahi kushiriki mashindano mbalimbali ya urembo nchini Husna Maulid, amesema uyatima umemfanya ayajue maisha mapema kwani mpaka sasa angekuwa hajaanza kujitegemea.

 

Akizungumza na SHUSHA PUMZI, Husna alisema kuwa kabla mama yake hajafariki alikuwa akimfanyia kila kitu, lakini alipotangulia mbele za haki, ndipo akili ilipotambua yuko peke yake na anahitaji kufanya awezalo ili maisha yaende.

 

“Baada ya kuwapoteza mama na baba nilikua mkubwa ghafla, kwa maana nilianza kukimbizana na majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko umri wangu na mpaka sasa nimekomaa kabisa na ninayajua maisha ipasavyo,” alisema Husna.

BEN POL ATAMBULISHA WIMBO MPYA WA ‘WAPO’ (PICHA +VIDEO)

Staa wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’ akisaini kitabu cha wagenialipotembelea ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam leo.

STAA wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’ leo alifika ndani ya ofisi za Global Group maalum kwa kutambulisha ujio wake mpya wa wimbo wa Wapo ambapo ameeleza namna mpenzi wake, Anerlisa,  alivyohusika katika kuandaa video ya wimbo huo.

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Richard Manyota (kushoto) akiongea jambo na Ben Pol.

Akizungumza katika Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio, Ben Pol alisema  kabla hajaachia wimbo huo mchumba wake huyo mwenye asili ya Kenya alikuwa halali akihakikisha video hiyo iwe nzuri.

Mtangazaji wa Global TV Online, Judith Mlwale (kushoto) akisalimiana na Ben Pol.

“Ane (Anerlisa) amenisaidia sana katika video hii ya Wapo. Nimekesha naye akihakikisha kila nguo ninayotumia kwenye video ipo sawa. Ana jicho zuri katika ubunifu kuanzia mimi,  hadi modo aliyetumika katika video ile amemtafuta yeye na kumvalisha,” alisema Ben Pol na kuongeza:

Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho,  akiongea jambo na Ben Pol.

“Aliku

Ben Paul akisoma meseji kabla ya kufanya mahojiano na Global Radio.