AMBER LULU KUMZALIA PREZZO!

VIDEO queen ambaye pia anafanya poa kunako Bongo Flevani, Lulu euggen ‘Amber Lulu’ amesema kwa sasa anaona kuwa hakuna cha kusubiri tena zaidi ya kumshauri mpenzi wake, Jackson Makini ‘Prezzo’ wazae mtoto.

Akizungumza na Amani, mrembo huyo alisema, anahitaji kuwa mama sasa kwani mambo ya usichana ameshayafanya sana.

“Nadhani huu ni muda wangu muafaka wa kuzaa, namshauri anayenimiliki tupate hata mapacha wa harakaharaka maana usichana nimeshafanya sana, nataka kuwa mama sasa  nibebe mtoto wangu ninyonyeshe,” alisema Amber Lulu

DAVINA AFUATA NYAYO ZA MOND

HALIMA Yahya ‘Davina’ ameonesha kufuata nyayo za staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’ kwa kuanzisha ‘brandi’ yake ya pafyumu. Mrembo huyo kutoka Bongo Movies ameliambia Amani kuwa, malengo yake makubwa ni kuhakikisha anafanya vizuri kwenye eneo la ujasiriamali kwani anaamini huwezi

kufanikiwa kama atategemea chanzo kimoja cha mapato. “Sanaa pekee haitoshi, nimekuja na pafyumu na losheni na kama unavyojua pia nina kampuni yangu ya kupika chakula, sishindani na mtu bali nafanya mambo yangu kuhakikisha tu ninakuwa na vyanzo vingi vya mapato,” alisema Davina. Mbali na Diamond, mastaa wengi kwa sasa wamejikita kwenye ujasiriamali kama huo akiwemo staa wa Bongo Fleva, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’.

Kim Kardashian Aamua Kumuonyesha Mwanaye kwa Mara ya Kwanza

MWANAMITINDO maarufu duniani Kim Kardashian ameamua kumuonyesha mtoto wake wa kiume kwa kuweka picha kwenye mtandao wake wa instagram kwa mara ya kwanza.

Mwanamitindo huyo kwenye kipindi chake cha runinga ‘Keeping up with Kardashians’, Kim Kardashian, alimuonesha mtoto wake huyo aliyezaliwa mwezi mei kwa njia ya mama mbadala na kumpatia jina la Psalm West.

Kim Kardashian ameweka picha ya mtoto huyo ikiambatana na ujumbe uliosomeka, ‘Psalm Ye’ Psalm likiwa na maana ya Zaburi.

Mimba ya Mpenzi wa Daimond Yazua Gumzo

ANAFICHA mimba! Ndivyo walivyosikika mashabiki waliomuona mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch kutokana na kuwa na tumbo kubwa hivyo kuibua gumzo kama lote kuwa ni mjamzito.

Mara kadhaa Tanasha amekuwa na kigugumizi juu ya suala la kuwa na mimba ya Diamond akisisitiza muda ukifika ataweka wazi.

Ishu hiyo iliibua gumzo kwa mara nyingine wikiendi iliyopita baada ya mrembo huyo kunaswa akicheza muziki na kunywa akiwa na Diamond katika kiwanja cha bata ndefu cha Ultra Gossip Lounge kwenye Majengo ya Lavington Mall jijini Nairobi, Kenya.

Mara tu baada ya kumuona, mashabiki hao mara moja walitoa simu janja zao na kuanza kurekodi video huku wakipiga kelele; “Anaficha mimba!”

Muda mfupi baadaye, video za tukio hilo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Tanasha akijitahidi kuficha tumbo lake ambalo lilionekana kuwa ni kubwa.

Mapema mwezi Aprili, mwaka huu, wakati akifanyiwa mahojiano na redio moja jijini Dar, Tanasha aligoma kusema chochote juu ya tetesi hizo kuwa ana mimba ya Diamond ambapo aliishia kusema; “Muda utasema.”

Hata hivyo, katika moja ya posti zake kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, Tanasha aliacha maswali mengi baada ya kudai kuwa anatarajia kupata baraka kubwa mno kwenye maisha yake ambapo bila kupepesa macho, watu waliunganisha nukta na kusema baraka hiyo ni mtoto wake wa kwanza atakayemzalia jamaa huyo.

“Jambo kubwa kwenye maisha yangu ni kwamba ninatarajia baraka kubwa hivi karibuni. Mungu ni mwema,” aliandika Tanasha bila kusema ni baraka gani hasa. Kwa wale wanaomfuatilia Tanasha kwenye ukurasa wake wa Instagram, hivi karibuni amekuwa akiposti picha za zamani tu, jambo ambalo limekuwa likiongeza mashiko kwenye tetesi hizo za kuwa ni mjamzito.

“Hivi ndivyo inavyokuwa mwili unapoanza kubadilika na uzito kuanza kuongezeka,” aliandika mwanadada huyo ambaye ni muuza sura kwenye video za wasanii, mwanamuziki na mtangazaji wa Kituo cha Redio NRG cha Mombasa, Kenya.

Wiki iliyopita, gazeti pendwa ndugu na hili, Amani linalotoka kila Alhamisi lilimtafuta Tanasha na kumbana juu ya mambo mbalimbali likiwemo suala hilo la kuwa mjamzito ambapo alijibu; “Napenda kuwaambia watu wasiamini kila wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye hizi kurasa za udaku na umbeya.”

Tukio la Tanasha kunaswa na kitumbo hicho kikubwa liliambatana na uzinduzi rasmi wa video ya Wimbo wa Inama wa Diamond aliomshirikisha mwanamuziki Fally Ipupa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ndani ya saa 16 tu baada ya kuzinduliwa Juni 9, video hiyo ilikuwa ina watazamaji (views) milioni moja kwenye Mtandao wa YouTube.

Ben Pol Afunguka Kuhusu Harmonize na Shetta Kumtumia Meseji Mpenzi Wake “Wala Sikushangaa”

STAA wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol, amefunguka kuhusu mambo kadhaa yaliyoibuka kwenye mitandao  kutokana na baadhi ya watu kudai kuwa amemfuma mpenzi wake, Anerlisa ‘Anna’, akiwasiliana na mastaa wa muziki nchini Tanzania akiwemo Harmonize na Shetta,  jambo ambalo lilidaiwa  huenda wanamtongoza bidada huyo ambaye ni raia wa Kenya.

Benpol anayetikisa na ngoma yake mpya ya WAPO aliyoiachia hivi karibuni baada ya ukimya wa muda mrefu, amesema hayo leo katika Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 10:00 jioni kupitia +255 Global Radio.

“Nakumbuka siku hiyo kuna kitu nilikuwa nafanya kwenye simu yake, ghafla ikaingia meseji DM ya Instagram, nikaingia nikawa naona majina ya mastaa wamemwandikia ujumbe, lakini nikaona hiki ninachokifanya sio kitu kizuri, hata kama ni mpenzi wako lazima umwachie privacy yake, huenda akawa anatafutwa kwa ajili ya biashara ama watu wengine wamemtumia proposal za kufanya naye kazi mbalimbali kwa sababu ni mjasiriamali.

“Kuandikiwa ujumbe na akina Harmonize wala haikunishtua kwa sababu ninamfahamu tabia zake, amekuwa akiandaa events mbalimbali na wao huwa wanakwenda sana kule (Kenya) kufanya shows kwa hiyo sikuona kama ni jambo la ajabu sana. Kuandikiwa ni jambo moja lakini ku-entertain ni jambo jingine.

“Hata mimi nilishawahi kupata kazi nyingi tu kupitia DM, sababu kupata namba mfano ya mkurugenzi wa kampuni flani inakuwaga ngumu sana, lakin DM ni rahisi kumpata mtu na ukawasiliana naye moja kwa moja, kwa hiyo niliona hilo jambo ni la kawaida sana wala watu wasifikiri labda Benpol alichukia, hapana. Watu wasione DM ni sehemu mbaya, hii ni sehemu nzuri kwa sababu inakuunganisha na watu tofauti.

Benpol livyokutana na mpenzi wake

“Mimi huwa nakwenda Kenya mara kwa mara, nilikwenda huko kwenye event moja, aliyenisaidia kuandaa event hiyo ni rafiki yake na Anna, baada ya event tukawepo tu tunapiga stori, akaniambia shughuli yake ‘nipo tu nauza maji’, sikutaka kuingia deep sana kuhusu kazi yake, tulibadilishana contacts, tukawa tunawasiliana, ninakwenda kule, tunatoka kidogo, tukapanga kufanya club tour, mimi nitangaze muziki wangu na yeye akawa anafanya activation ya maji yake, na baadae akaja Tanzania.

Baada ya miaka 27 Mary J Blige kutunukiwa tuzo ya heshima na BET

Inaripotiwa kuwa Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Pop na RnB ambaye pia ni muigizaji Mary J. Blige’48 inaelezwa kuwa atatunukiwa tuzo ya heshima (Lifetime Achievement Award) kwenye tuzo za BET zitakazofanyika June 23, 2019.

Inaelezwa kuwa mwimbaji huyo ambaye aliwahi kuwa mshindi tuzo za Grammy mara tisa pamoja na kuuza album zake mara nane (multi-platinum) atatunukiwa heshima hiyo kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye tasnia ya muziki tangu mwaka 1992 nchini Marekani.

Mary Blige  ataungana na waimbaji kama Anita Baker wa mwaka jana, pia Charlie Wilson, Diana Ross, Whitney Houston, New Edition, James Brown na Prince wakiwa miongoni mwa mastaa waliopokea tuzo hiyo ya heshima